Kuhifadhi maziwa

Chukua chupa ambazo ni safi kabisa, nzuri na kavu. Kamua maziwa toka kwa ng’ombe na yajaze kwenye chupa. Baada tu ya kujaza maziwa kwemye chupa, funika haraka chupa kwa kizibo au mfuniko wake, halafu kaza kwa uzi ama waya. Kisha weka ukili/nyasi/matete/straw chini ya kifaa cha kuchemshia, ambapo utaweka chupa zako zikiwa zimetenganishwa na ukili/nyasi/matete/straw hiyo.

Idadi ya chupa iwe ya kutosha kifaa chako cha kuchemshia. Jaza kifaa chako cha kuchemshia maji ya baridi (chupa za maziwa zikiwemo ndani) na pasha joto, punde tu maji yatakapoanza kuchemka ondoa moto, na acha vyote vipoe taratibu. Na vikishakuwa baridi kabisa toa chupa zako, na zifungashe kwa kutumia mirija au maranda ndani ya makasha na hifadhi sehemu baridi kuliko zote kama ni kwenye nyumba ama meli.

Maziwa yaliyohifadhiwa kwa njia hii, ingawaje miezi 18 kwenye chupa tangu kukamuliwa, yanakuwa matamu na mazuri kama yamekamuliwa muda huo (fresh).

Ukurasa huu ni kipisi tafadhali saidia kuendeleza!

FA info icon.svg Angle down icon.svg Page data
Authors Christopher Sam
License CC-BY-SA-3.0
Language Kiswahili (sw)
Translations Kiingereza
Related 1 subpages, 1 pages link here
Impact 910 page views
Created Mei 5, 2011 by Christopher Sam
Modified Novemba 15, 2022 by Felipe Schenone
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.