Je wiki kama Appropedia, ni ya kazi gani kwa masikini ambao hawana mtandao?
- Nani hana internet?Sio wengi kama unavyofikiri –mgawanyiko wa kidigitali unavukwa kwa haraka katika nchi zinazoendelea zaidi ya ilivyotekea katika nchi zilizoendelea.
- Safiri katika nchi iliyoendelea kidogo na haswa utaona vibanda vya internet, na utumiaji ulioenea wa simu za mikononi. Hii haifikii kila mtu,lakini inachukua watu wachache kwa mawazo kuenea, na namba ya watu walio na fursa inaongezeka.
- Kuruka hatua: Watumiaji wanaruka matumizi ya laptop, na simu zinakuwa janja kwa haraka.
- Simu: Hadithi ilielezwa katika BarCampAfrica[1] juu ya mazungumzo Africa. "Umesikia juu ya Google?" "Ndio, kabisa." "Umetafuta na Google kwa simu yako ya mkononi?" "Kabisa –ni kipi tena unaweza kutafuta na Google?" Unahitaji simu moja tu kijijini yenye uwezo huu kuongeza kwa kiwango kikubwa uwezo wa watu kupata taarifa.
- Simu janja zinauza zaidi ya simu jinga Africa tayaria.[2]
- Gharama za matumizi ya kompyuta zinaendelea kuanguka kwa karibu nusu kila baada ya miaka miwili,hii inajulikana kama kanuni ya Moore.W Athari ya kanuni ya Moore ni kwamba waendelezaji wa mfumolaini na maudhui mara chache wanahitajika kufikiri juu ya kumudu bei ya mfumomgumu. Waendelezaji kwa urahisi wanaweza wakajenga aplikesheni zao, wakijua kwamba punde ama baadae mihadhara lengwa itaweza kumudu kompyuta kuendesha aplikesheni zao. Mwishowe gharama za matumizi ya kompyuta zitakuwa chini zaidi ya chakula, kuweka kompyuta ndani ya bajeti ya mtu yeyote ambaye amemudu kukaa hai.
- Katika mwezi, Appropedia inapata wageni/watumiaji toka katika kila nchi isipokuwa katika nchi 4 au 5 (mara nyingi ikijumuisha North Korea and Greenland).
- Tunajaribu kufanya tovuti hii nyepesi, na watumiaji wanaweza kuchagua ukubwa wa picha wanazoziona. Kama unaweza kutusaidia kuboresha "bandwidth yetu nyepesi" zaidi, tutafurahi sana.
- Kuna njia nyingi za kueneza offline content, kama vile:
- Katika kompyuta (e.g. Appropedia's offline content bundle & Appropedia:Offline browsing), CD-ROMs, DVDs, flash drives, hard drives
- Kuchapa kama vipeperushi, vijitabu au vitabu – kwa mfano tumia kiunganishi cha "Create a book" kilichoupande wa kushoto wa navbar. (Hii ni sababu moja muhimu sana ya kutumia open license inayoruhusu matumizi ya biashara, ili biashara ndogondogo katika nchi zinazoendelea zihamasike kutawanya maarifa haya.)
- Programu za elimu katika jumuiya juu ya maudhui yaliyomo katika wiki. Hii ni sababu moja jumuiya ya Appropedia inaendeleza maudhui ambayo ni muhimu kwa aid and development workers na wafanyakazi wa community development wa ndani.
- Wanavijiji waliohamia kwenye majiji kufanya kazi, ambao wanabakiza uhusiano na kijiji – kama wana uwezo wa kuwa na mtandao, wanaweza kutaarifiwa, na kupeleka ama kutuma taarifa kwenye vijiji.
- Njia hiyo nyingine – ambayo sisi wote bado hatujaifikiri.
- Tunahitajika kuendeleza taarifa, rasilimali, na kuweka jitihada zaidi katika uenezaji.
- Appropedia inaweza kusaidia masikini ambao hata hawajawahi kuiona, kwa kuwafundisha matajiri kuishi katika njia zinazopunguza madhara kwa masikini. Kwa mfano, Appropedia inaweza kuhamasisha matajiri kupunguza alama ya hewa ukaa, kwa hivyo kupunguza mabadiliko ya tabianchi jambo ambalo ndio tishio kubwa pekee linalokabili nchi zinazoendelea.
Notes[edit | edit source]
- ↑ Mountain View, CA, USA, 2008
- ↑ http://whiteafrican.com/2009/08/25/should-we-be-building-sms-or-internet-services-for-africa/