Takataka zinabaguliwa ambapo zile zenye nyuzi zaidi zinatumika kutengenezea Makaa/briketi. Picha kwa msaada wa greenlivingproject.com

Makaa ni fueli rafiki wa mazingira na chanzo mbadala cha nishati kinachotumika Kigali, Rwanda.

Kwa ufupi[edit | edit source]

Katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, uchafu wa mtu mmoja hakika ni fueli rafiki wa mazingira kwa mtu mwingine. Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo unasimamia mradi wa jumuiya ambao unafanywa pamoja na Franciose Kayigamba. Mama huyu ni Mratibu wa kitaifa wa mradi wa GEF (Global Environmental Facility) ambao unafanikisha mradi huu wa jumuiya. Mchakato huu unahusika na kubadilisha takataka kuwa nishati endelevu inayojulikana kama makaa/briketi.

Jinsi gani Makaa/briketi yanatengenezwa[edit | edit source]

Rwanda ndio nchi iliyo na uwiano mkubwa zaidi wa watu katika eneo barani Afrika na zaidi ongezeko la idadi ya watu linaongeza msongo zaidi katika mazingira. Kitu chochote kuisaidia Rwanda kuelekea uendelevu ni njia sahihi. Katika mji mkuu wa Kigali, kuni na mkaa ndio fueli zinazoongoza kwa kutumiwa katika kupikia na kupasha joto na Rwanda vijijini kuni ndio chanzo kikuu cha fueli. Katika nchi zinazoendelea kuni ndio chanzo kikuu cha fueli. Utegemezi huu mkubwa wa fueli ya kuni katika kupikia na kupashia joto unasababisha matatizo makubwa ya kimazingira Rwanda, kwa mfano uchafuzi wa mazingira na ukataji wa miti.

Kikundi cha wanawake, ACEN/COOCEN, ndio kinahusika na mradi wa kubadilisha takataka kuwa makaa/briketi ya kiikolojia. Hali hii itapunguza hewa ukaa (CO2) na ukataji miti. Takataka za nyumbani zinakusanywa toka familia 12,000 za Rwanda na zinapelekwa katika mitambo iliyoko Kigali. Hapo, vitu vyenye nyuzinyuzi kama vile kamba za miti, manila/karatasi ngumu, karatasi, mboji na vipande vidogovidogo vya vinakusanywa, vinakaushwa na kugandamizwa. Na hapo vinabadilishwa kuwa makaa/briketi ambayo yanafanya kazi sawa na kuni lakini yanaungua kwa usafi na yana ufanisi zaidi katika matumizi. Tani kumi na nne za makaa/briketi zinatengenezwa kila siku. Na yanauzwa kwenye shule, jela, viwanda n.k na hayatumiki sana nyumbani.

Majiko ya makaa/briketi[edit | edit source]

Makaa ni rahisi na rafiki wa mazingira na pia ni mbadala wa kuni na mkaa. Picha kwa hisani ya greenlivingproject.com

majiko ya kawaida ya nyumbani yanaweza kutumika wakati wa kutumia makaa/briketi kama fueli katika maisha ya kila siku. Majiko haya yatanyanyua matumizi ya makaa/briketi katika kaya. Takribani dola za marekani 25, au franka za Rwanda 14,000 zinatumika kununulia mkaa kila mwezi Kigali. Kwa kutumia makaa/briketi na majiko ya briketi gharama zinapungua mpaka chini ya dola za marekani $8 au franka za Rwanda 2,000 kwa mwezi. Jiko la makaa/briketi lingharimu kiasi cha dola za marekani 15-28 US.

Matokeo[edit | edit source]

matokeo ya uzalishaji huu wa makaa/briketi unaboresha uendelevu Rwanda. Kwanza, yanapunguza kiwango cha takataka kwa ujumla, gesi za methane na yanatia chachu katika uhifadhi wa takataka. Pili makaa ni rahisi zaidi ya mkaa na kuni na kikundi husika kimetengeneza ajira zaidi ya 100 na asilimia 90% ya wanufaikaji ni wanawake.

Angalia pia[edit | edit source]

Faharasa[edit | edit source]

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.