FA info icon.svg Angle down icon.svg Project data
Location Tanzania
Made No
Replicated No
OKH Manifest Download
FA info icon.svg Angle down icon.svg Device data
Hardware license CC-BY-SA-4.0
Certifications Start OSHWA certification

Kuua vijidudu kwenye maji kwa Jua, pia inajulikana kama solar water pasteurisation au SODIS, ni njia ya kuua vijidudu kwenye maji ya kunywa kwa kutumia nishati ya joto na miali ya UV toka kwenye jua. Ni njia rahisi sana na ya Gharama nafuu ya kuua vijidudu katika maji ya ujazo mdogo.

Minunurisho katika spektramu/spectrum ya UV-A (mawimbi/wavelength 320-400nm) na ongezeko la joto la maji. Mambo yote haya yanaharibu vinasaba/DNA za vijidudu. Matokeo ni kwamba vinasaba/DNA hivyo vinaharibiwa kirahisi kama jotoridi ni kali sana. Kama jotoridi litaongezeka juu ya 50°C, uuaji vijidudu unaharakishwa mara tatu zaidi, na matokeo mazuri zaidi yanapatikana toka kwenye miali ya UV.

Ila vijidudu kama vile Giardia,W, haviuliki kirahisi kwa UV. Kwa hivi, joto ni muhimu/kuchemsha maji.[verification needed]

Matumizi[edit | edit source]

  • Weka akilini kwamba SODIS ni njia ya kuua vijidudu tu, na sio njia inayokamilisha usafishaji wa maji. Kama maji ni machafu sana, hatua za ziada ni lazima[1] - kwa mfano uchujaji wa kutosha kabla ya kuweka maji yapigwe na miali ya UV.

SODIS: chupa za soda na mwanga wa jua[edit | edit source]

Kuua vijidudu kwenye maji kwa Jua, au SODISW, ni njia ya kuua vijidudu kwenye maji kwa kutumia mwanga wa jua na chupa za PET/chupa za plastiki zisizo na rangi ambazo unaweza kuona pande moja hadi nyingine.

  • Maji toka kwenye vyanzo vilivyoingiliwa na vijidudu yanajazwa kwenye chupa za plastiki zinazoonesha. Kwa kiwango kikubwa cha oksijeni, chupa zinajazwa maji kwa kiwango cha robo tatu, ni kisha zinatikiswa kwa sekunde 20 (mfuniko ukiwa umefungwa), halafu zinajazwa mpaka juu. Maji machafu sana (hali ya tope juu ya 30 NTU) ni lazima yachujwe kabla ya kuwekwa juani.
  • Sasa chupa zilizojazwa zinawekwa juani. Matokeo mazuri ya halijoto yanapatikana kama chupa zitawekwa juu ya mabati na sio juu ya mapaa ya nyasi.
  • Maji yaliyopitia mchakato huu yanaweza kutumiwa. Hatari ya maji kuingiliwa na vijidudu tena inaweza kupunguzwa kwa kuhifadhi maji kwenye chupa husika. Maji yatumike moja kwa moja toka kwenye chupa au yamiminwe kwenye vikombe visafi. Kujaza maji katika vyombo vingine kutaongeza hatari ya kuingiliwa upya na vijidudu.

Matokeo yanaweza kuboreshwa kwa kuweka chupa juu ya sehemu nyeusi ama zinazoakisi mwanga, mfano.

  • mabati ya kuezekea.
  • au kwa kuzipaka chupa rangi nyeusi nusu, hili zitakapowekwa juani nusu iliyobaki itazame anga.

Kutumia viakisi[edit | edit source]

Enhancement of Solar Water Pasteurization with Reflectors, Negar Safapourdagger and Robert H. Metcalf, 1998, Department of Biological Sciences, California State University Sacramento, Sacramento, California.

Njia hii inatumia manila na jagi jeusi. Joto ndio njia inasemwa na waandishi kuwa inafaa na ya kutegemewa ya kuua vijidudu.

Angalia pia: CPCs

Historia[edit | edit source]

Profesa Aftim Acra wa Lebanon ndie aliyetafiti ujuzi huu kuanzia 1979. Angalia Cleaning water with sunshine, Robert Bourgoing, IDRC Reports, April 1989. (or the original format with image, in PDF.) See also An Interview with Aftim Acra, Professor Emeritus of Environmental Sciences, Winter 2004.

Angalia pia[edit | edit source]

Viunganishi katika wiki[edit | edit source]

Viunganishi vya nje[edit | edit source]

Viunganishi vya miradi[edit | edit source]

Faharasa[edit | edit source]

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.