3 stage communal water filter.png
FA info icon.svg Angle down icon.svg Project data
Authors Christopher Sam
Made No
OKH Manifest Download

Makala hii inahusika na uundaji wa mfumo wa kuchuja maji wa gharama nafuu sana. Uchujaji maji unaweza kufanyika kama kuna njia chache ama hakuna kabisa njia mbadala za kupata maji safi toka vyanzo vingine kama vile maji ya mvua, maji ya ardhini (na sio yatembeayo juu ya ardhi), ... Kama uchujaji maji hauhitajiki kabisa basi kwa ujumla gharama huwa nafuu, na pia kunakuwa na kukwepa kwa utumiaji wa nishati ( na uwezekano wa uchafuzi wa hewa). Mambo yatategemea mazingira husika lakini (uwepo wa vyanzo vya maji).

Dhumuni[edit | edit source]

Sehemu ya kusafishia maji yawekwayo kwenye samaki
Chujio la maji ya jumuia

Kama ilivyoelezwa dhumuni la kuunda mfumo huu wa gharama nafuu ni kusafisha maji yawe masafi bila chembechembe za udongo au uchafu mbaya. Kama maji ni kwa ajili ya kunywa, yachemshe katika nyuzi joto 100 kwa dakika 5 na kama huko kwenye vilele basi chemsha kwa dakika saba.[1] Hii inahitajika na inashauriwa kutokana na sababu za Afya ya jamii-lakin kuchemsha maji katika nyuzi joto juu ya 70 kutaua vijidudi vingi [verification needed] hasa kama joto hilo litaendelezwa kwa kipindi. Vinginevyo unaweza kutumia maji kama yalivyo kama vile kwa ajili ya ufugaji samaki au tumia jua kuyafukiza

Muundo[edit | edit source]

Kutokana na vifaa vya chujio: kuna majani, mchanga na mkaa. Kifaa cha kwanza (majani) kinachuja chembechembe zote kubwa za udongo au mchanga. Mchanga pia unafanya kazi kama chujio au chekeche kama majani yanavyofanya. Muhimu, ninaote kwamba majani yalichukuliwa kama chujio la awali kwani yanapatikana kwa gharama nafuu na yanapatikana kiurahisi kuzidi mchanga na hivyo yanaweza kubadilishwa mara kwa mara. Mwishoni mkaa ndio chuji la tatu na ndilo chujio lenye ufanisi zaidi, mkaa unaweza kuchuja chembechembe ndogo kabisa na baadhi ya viumbe hai (bacteria); lakini kwa namna yeyote ile chemsha maji.

Chujio la Tengeneza mwenyewe ni kwa ajili ya dharura kali; linaweza kutumika katika mazingira ya kijiji, yaani, hasa katika maeneo maskini sana, kusikokuwa na upatikanaji wa vifaa vya ujenzi. Lakini, mfumo utakaokuwa umetengenezwa kwa ajili ya matumizi ya jumla ni vizuri uwe wa ndani: mfumo huo utakuwa endelevu zaidi na rahisi kumudu. Kama visafishi zaidi vitaongezwa, basi maji yanaweza kufanywa kuwa masafi zaidi.

Kufanya maji yawe masafi zaidi, angalia Treatment pond na http://en.wikipedia.org/wiki/Rainwater_harvesting (ya mwisho ni juu ya uvunaji wa maji ya mvua, lakini inajumuisha mifumo au maelezo juu ya uundaji wa machujio ya maji ya ndani pial)

Angalia pia[edit | edit source]

Faharasa[edit | edit source]

FA info icon.svg Angle down icon.svg Page data
Keywords water filter, purification, chujio la maji
SDG SDG10 Reduced inequalities, SDG11 Sustainable cities and communities, SDG02 Zero hunger, SDG09 Industry innovation and infrastructure
Authors Christopher Sam
License CC-BY-SA-3.0
Language Kiswahili (sw)
Related 0 subpages, 1 pages link here
Impact 601 page views (more)
Created Machi 27, 2011 by Christopher Sam
Last modified Juni 8, 2023 by Felipe Schenone
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.