Umeme ni aina mojawapo ya nishati ambayo inatokana na utembezi wa chembechembe(electrons?) katika sakiti. Umeme hutumika majumbani na viwandani katika kufanya shughuli maalum. Majumbani umeme hutumika kama chanzo cha mwanga(kuwasha taa), kutoa sauti na picha(kuendesha redio na runinga)joto(kupiga pasi na kupikia) na nguvu za kimakanika kama kuzungusha mota. Vyanzo vya umeme ni pamoja na upepo, mafuta, gesi, jua, nyuklia na kemikali.

Aina za mikondo ya umeme[edit | edit source]

Kuna makundi makuu mawili ya umeme, ambayo ni umeme mkondo mnyoofu na umeme usio mkondo mnyoofu. Aina hizi mbili zote ni muhimu kutegemeana na matumizi na upatikanaji wake.

Matumizi na miundo[edit | edit source]

Baada ya umeme kuzalishwa hupaishwa volti zake na kuwekwa katika gridi ya taifa. Hupaishwaji huu wa volti hufanyika ili kupunguza hupotevu wa umeme katika hali ya joto. Umeme huu ili uweze kutumika majumbani transfoma hutumika kushusha volti kufikia 240/340. Kutokana kuungezeka kwa kasi kwa idadi ya watu na viwanda nchi nyingi zinaelekea kushindwa kumudu mahitaji ya umeme na haswa nchi zinazoendelea.

Vyanzo[edit | edit source]

Nchi nyingi zinazoendelea zinategemea umeme wa maji , gesi na mafuta. Lakini hata hivyo vyanzo hivi havitoshelezi kutokana na mitambo kuzeeka na kuwa ya kizamani. Pia umeme wa gesi na mafuta ni aghali na nchi nyingi zinazoendelea zinashindwa kumudu. Kutokana na tatizo la kuongezeka kwa joto duniani inashauriwa kutumia vyanzo kijani vya umeme kama vile upepo, jua na nguvu za mtu ama mnyama. Vyanzo hivi ni salama kwani havitoi hewa ya ukaa(kaboni) ama kemikali zenye sumu. Pia kama mipango madhubuti itafanyika kabla ya kuchagua kutumia vyanzo hivi basi gharama itakuwa ni nafuu na mitambo itadumu kwa muda mrefu. Mara nyingi vyanzo hivi huonekana kuwa na gharama kubwa lakini ukweli ni kwamba kwa muda mrefu gharama zake ni ndogo ukilinganisha na vyanzo vingine. Na pia vyanzo hivi mara nyingi haviathiriwi na mfumuko wa bei kwa mfano pale mafuta yanapopanda bei.

Umeme unaosambazwa majumbani na viwandani hulipwa kwa KWh, yaani idadi ya wati elfu moja katika saa moja ama unaweza kusema pia idadi ya wati elfu moja zilizotumika katika saa moja. Kimahesabu KWH inapatikana kama ifuatavyo;


Kiasi=Nguvu × muda ; ambapo nguvu inapatikana kwa, Nguvu=Volti × karenti(mkondo wa umeme uliopita).

Mfano Kama utatumia jagi la umeme lililoandikwa(mara nyingi upande wa chini) 2000W, 240V kwa muda wa dakika tano basi hutakuwa umetumia kiasi au KWH zifuatazo. Kiasi=Nguvu × muda Kiasi=2000W × dakika 5.

Lakini kumbuka ili tuweze kupata jibu sahihi ni lazima tuzibadilishe dakika tano ziende katika saa na 2000W katika KW(yaani wati gawanya kwa elfu moja) kama kanuni inavyoelekeza, hivyo tutakuwa na		

Kiasi= 2KW × 5/60h Kiasi=0.167KWh. Kama gharama ya umeme ya sehemu husika ni Tshs 129 kwa 1KWh basi kwa dakika hizo tano ulizotumia jagi lako la umeme itakugharimu; Gharama=KWh zilizotumika × bei =0.167 × 129 =21.54Tshs Hivyo matumizi hayo yatakugharimu shilingi ishirini na moja na senti hamsini na nne.

Discussion[View | Edit]

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.