Kuna wakati katika shughuli za kawaida inatokea bahati mbaya na simu ya mkononi inatumbukia kwenye maji na kulowa. Unaweza kujiepusha na hili lakini kwa kuwa kulowa hutokea kama ajali basi ikiwa simu yako ya mkononi imetumbukia kwenye maji na kulowa, fanya yafuatayo:

Hatua[edit | edit source]

Zima simu kama baada ya kulowa au kutumbukia kwenye maji haikuzima yenyewe. Toa mfuniko wa betri na betri. Toa kadi ya simu. Kisha kwa uangalifu toa mfuniko wa kicharazio na kicharazio. Baada ya haya chukua kipande cha godoro ama kitambaa kisichotoa na kuacha nyuzinyuzi kwa urahisi na pangusa taratibu sehemu za simu yako ili kunyonya maji yaliyolowesha. Ukimaliza zoezi hili unaweza kuanika sehemu za simu yako juani ama ukaziweka sehemu za simu yako juu ya mchele mkavu(ambao haujapikwa). Mchele utafyonza unyevunyevu wote. Unaweza kufanya haya kwa muda wa dakika ishirini hivi.

Usomaji zaidi[edit | edit source]

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.