Maana

Umeme jua ni nishati ambayo chanzo chake ni mwanga wa jua. Nishati hii huzalishwa pindi miale ya jua inapoangaza seli za fotovoltaiki. Seli za fotovoltaiki huzalisha umeme mkondo mnyoofu ambao huifadhiwa kwenye betri. Umeme jua huifadhiwa kwenye betri ili kumuwezesha mtumiaji kupata nishati wakati wa usiku pia ambapo kunakuwa hakuna mwanga wa jua. Pia nishati iliyohifadhiwa kwenye betri ni muhimu wakati wa mawingu na mvua nzito ambapo uzalishaji wa nishati unakuwa mdogo. Umeme jua ni aina mojawapo ya nishati hai.

Template:Kipisi

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.