Tafsiri[edit | edit source]

Betri ni muunganiko wa seli zaidi ya moja. Muunganiko huu unaweza kuwa ni wa moja kwa moja tokea kiwandani kama vile katika betri za gari na pikipiki, au muunganiko wa nje kama vile seli kavu katika redio.

Aina[edit | edit source]

Tunaweza kuainisha betri katika makundi makuu mawili, yaani betri za sekondari na betri za awali. Betri za sekondari zina uwezo wa kuchajiwa baada ya kutumika. Na mzunguko huu unaweza kuwa ni wa miaka mingi. Betri za awali haziwezi kuchajiwa baada ya kutumika. Mara nyingine hali hii imepelekea betri hizi kuitwa betri za kutupwa. Kutokana na sababu za kimazingira na ufinyu wa rasilimali betri hizi zimeanza kupoteza umaarufu.

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.