Get our free book (in Spanish or English) on rainwater now - To Catch the Rain.

Pampu ya koili

From Appropedia
Jump to: navigation, search
Kiswahili - English
Pampu ya koili; muhimu kujua pampu hii ni ya msingi na haijawekewa spirraling pattern (?), hii inaweza kuwekwa lakini

Pampu ya koili ni pampu ya unyanyuaji wa chini inayoundwa na tyubu/neli/bomba, iliyoundwa katika mfumo wa koili na kuungwa katika ekseli inayozunguswa na injini ama mnyama aliye na uwezo wa kuzungusha ekseli kwa haraka. Kutokana na mzunguko, maji yanachotwa na bomba/tyubu/neli na kusukumwa juu kupitia mpira wa maji.

Matumizi[edit]

Pampu ya koili, kama pampu nyingine nyingi za unyanyuaji wa chini, inatumika sana katika umwagiliaji na ukaushaji wa ardhi. Kwa sasa bado inatumika na wakulima walioko Asia.[1]

Faida[edit]

Pampu ya koili iliundwa kwa ajili ya kuwa mbadala wa Archimedean screw. Tofauti na Archimedean screw, hii inaweza kuendeshwa katika mlalo ambapo Archimedean screw inalazwa katika 30° hivi. Pampu ya koili, kama itawekewa sili nzuri inayozunguka, inaweza kupeleka maji katika kimo kirefu zaidi, hasa 5-10m, juu ya sehemu yake ya kutolea maji.[2]Bila kujali kutokea kwa pampu mpya zinazofanya kazi katika kanuni nyingine tofauti, pampu ya koili inabaki kuwa kifaa muhimu kwa kuwa moja ya faida zake ni ujenzi rahisi na marekebisho ya gharama nafuu. Hii inawezekana kwa sababu vifaa vyote vinaweza kuundwa kwa kutumia mali za ndani kama metali; ambayo inaweza kupatikana na kufuliwa katika umbo linalohitajika kirahisi.

Hasara[edit]

Kama ilivyotajwa awali, pampu ya koili inaruhusu unyanyuaji maji katika kimo kidogo. Hali hii inaifanya isifae kutumika katika ukaushaji maji au umwagiliaji katika maeneo yenye utofauti mkubwa wa kimo au matumizi mengine mengi ya usukumaji tofauti na umwagiliaji na ukaushaji wa maeneo.

Faharasa[edit]

Angalia pia[edit]