Nini na kwanini[edit | edit source]
Pampu za mikono za viwandani kama vile Indian mark II, kwa ajili ya visima vya vijiji za msaada toka miradi ya maendeleo mara nyingi huaribika baada ya miaka miwili.
Kama gharama za matengenezo ni juu ya watumiaji basi itakuwa ni aghali sana wakati ambapo ukarabati ni lazima na pampu haifanyi kazi. Pampu mbadala ya mkono inayotegemeka inahitajika kwa ajili ya matumizi ya jamii na binafsi ili kutoa maji safi ya kunywa na kumwagilia. Pampu hizi zitainua hali za maisha kama gharama zake ni ndogo, zinategemeka na zinapampu maji kwa ufanisi. Ufanisi ni muhimu wakati wa umwagiliaji bustani kipindi cha kiangazi kutokana na kiasi kikubwa cha maji kinachohitajika. Bustani kama hizi zinatoa chakula na kuongeza kipato. Kumudu gharama kwa jamii husika na matengenezo ya pampu ya kamba.
Vipi[edit | edit source]
Sehemu ya mnyororo inachukuliwa na kamba halafu gurudumu lizungushwalo na mnyororo likibadilishwa na gurudumu lililotengenezwa kwa mpira. Gurudumu hili la mpira linaweza kutengenezwa toka kwenye tairi la gari lililokwisha tumika. Vifaa vingine vinavyohitajika vinaweza kupatikana kwa gharama ndogo ama bure. Muda mdogo unahitajika kuwaelekeza watumiaji ama waashi jinsi ya kutengeneza pampu ya kamba. Watu wanaasili kanuni kuu kutokana na mahitaji yao, kama ni visima vifupi ama virefu kama ni visima vya chini ama maji toka mabwawani. Kupata ubora unaoelekezwa lazima kuzingatia uhusiano baina ya kipenyo cha gurudumu na kipenyo cha bomba la plastiki la pampu. Kwa nyongeza ujenzi sahihi wa mahali ambapo kamba inabadili muelekeo toka chini kwenda juu ya kisima ni muhimu. Kama maelekezo juu ya ubora yatafuatwa, pampu ya kamba inashinda pampu iliyozoeleka kwa kiwango kikubwa zo na ufanisi mzuri Pampu ya kamba ya demotech ni bora katika nyanja zote za matumizi na kwa bei ukilinganisha na pampu nyingine za mkono. Maboresho zaidi yatamaanisha kupunguza nusu ya gharama, ikiifanya kufaa kwenye visima vya kina cha 100mita, matengenezo ya haraka na ufanisi, ujenzi madhubuti na kuzungushiwa nyumba(housing) na pia kusukuma maji mengi zaidi na ufanisi zaidi. Pampu ya kamba inaweza kuasiliwa kwa matumizi maalum. Kuifanya ifae kusimamishwa juu ya mfuniko wa kisima, beringi ya ekseli ya pampu inawekwa kwenye upande wa gurudumu la pampu tuu. Katika miundo mingi mingine huwa inachaguliwa kuweka beringi katika pande zote mbili za gurudumu la pampu.
Vyanzo vingine[edit | edit source]
- http://web.archive.org/web/20100927043751/http://rdic.org/home.htm
- http://web.archive.org/web/20141012082452/http://ideas-at-work.org/index.html