Utangulizi[edit | edit source]

Katika maisha ya sasa simu ya mkononi ni kifaa muhimu sana kwani mbali na kuwezesha mawasiliano, simu za mikononi hutumika kama vipashio vya habari(kupitia redio, huduma ya ujumbe mfupi, n.k), kutoa burudani na huduma za fedha. Kutokana na haya ni muhimu kufahamu namna ya kuwezesha simu yako kudumu na chaji muda mrefu na pia kurefusha maisha ya betri ya simu yako.

Hatua[edit | edit source]

  • Ili kuwezesha maisha marefu ya betri ya simu yako fanya yafuatayo.
    • Hakikisha unazima simu yako wakati wa usiku(ukiwa unalala) kama hautegemei simu muhimu wakati huo.
    • Ukichaji simu yako hakikisha umepata maelekezo ya betri kujaa, yaani 'battery full'. Na ikiwa utegemei kupokea simu wakati huo basi simu izimwe wakati wa kuchajiwa.
    • Hakikisha visaidizi kama tovuti, BLUETOOTH na INFRARED vimezimwa kama havitumiki. Kama visaidizi hivi vitakuwa vimewashwa(ON) vitanyonya chaji ijapokuwa hauvitumii.
    • Hakikisha hautumii screen saver angavu ama yenye kubadilikabadilika. Rangi nyeusi au NO/NONE katika 'screen sever' ni bora zaidi.
    • Pia hakisha unaweka muda mdogo kabisa wa backlight/uangavu na screen saver time out/muda wa screen saver kuanza.
    • Epuka kubofya simu yako kama hakuna jambo la msingi unalofanya.
    • Kama uko kwenye mazingira yenye taabu ya umeme basi epuka kucheza michezo.
    • Kama mlio wako wa simu unasikika vizuri basi zima mtetemo/vibration.
    • Na kumbuka kuzima simu yako mahali kusiko na mawimbi/network. Simu hutumia chaji nyingi sana ikiwa inatafuta mawimbi.
    • Pia kumbuka kutohifadhi simu yako maeneo yenye joto kali.
FA info icon.svg Angle down icon.svg Page data
Authors Christopher Sam
License CC-BY-SA-3.0
Language Kiswahili (sw)
Related 0 subpages, 0 pages link here
Impact 463 page views
Created Juni 21, 2011 by Christopher Sam
Modified Novemba 15, 2022 by Felipe Schenone
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.