Page data
Authors Christopher Sam
Published 2011
License CC-BY-SA-4.0
Impact Number of views to this page. Views by admins and bots are not counted. Multiple views during the same session are counted as one. 332

Kapasita|kwa kiswahili(capacitor, in english). Kapasita ni kifaa kitumikacho kukusanya na kuhifadhi umeme. Katika muundo rahisi kabisa kapasita inaundwa na visahani viwili vya metali vinavyotenganishwa na maada isiyopitisha umeme, yaani daielektriki.

Uwezo wa kapasita kuhifadhi umeme ujulikana kama kapasitensi kifupisho ni C. Na kipimo chake katika mfumo wa kimataifa wa vipimo ni Faradi, kifupisho ni F. Lakini faradi 1 ni kubwa sana ivyo vipimo vidogo vya (1/1000)F=MFD, -1/1000000)F=NFD, (1/1000000000)F=PFD hutumika. Kimahesabu kiwango cha chaji kilichohifadhiwa na kapasita hupatikana kwa Q=CV, ambapo Q ni chaji, C ni kapasitensi na V ni volti. Kapasita ni kifaa muhimu sana katika vifaa vya elektroniki. Mbali na kuhifadhi umeme kapasita hutumika kusawazisha volti au mkondo wa umeme upitao. Pia kapasita hutumika kutambua mawimbi ya umeme, kama kwenye redio-kutafuta masafa ya redio mbalimbali.

Ukurasa huu ni kipisi tafadhali saidia kuendeleza!