Ampia (in english ampere) ni kipimo cha mfumo wa kimataifa cha vipimo cha kiasi cha mkondo wa umeme upitao katika sakiti. Kifupi chake ni A. Vifaa vingi vya umeme vya majumbani huwa vimeandikwa kiasi cha ampia zinazohitajika ili kifaa kiweze kufanya kazi. Kama mkondo utakuwa pungufu basi ni dhahiri kifaa kitashindwa kufanya kazi au kitafanya kazi lakini si kwa ufanisi. Na pengine hata kuharibika.

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.