Tafsiri
Asali inaweza kusemwa kama kimiminika chenye ladha tamu ya sukari, chenye kunata na rangi ya manjano.
Matumizi
Chakula
Asali hutumika kama chakula, pia kama kiongezeo katika vyakula kama mkate, karanga na nafaka nyingine.
Matibabu
Katika sehemu nyingi duniani watu wanatumia asali katika kutibu magonjwa mbalimbali lakini pia katika kuongeza kinga ya mwili.
Lishe katika Asali
Asali ni chanzo sahihi sana cha wanga kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na nishati.
Urinaji Asali
Njia za jadi
Historia inaonesha urinaji asali umekuwapo kwa kipindi kirefu. Na njia ambazo zimekuwa zikitumika ni za jadi, kutoka na ubunifu asilia. Muhimu kufahamu njia hizi zimeendelea kutumika hadi sasa.
Njia za kisasa
Njia za kisasa zinazingatia utaalam katika kurina asali. Njia hizi huleta tija kutokana na kuzalisha asali kwa wingi katika eneo dogo.