{"id":39100,"key":"Asali","title":"Asali","latest":{"id":1247441,"timestamp":"2026-05-12T18:18:54Z"},"content_model":"wikitext","license":{"url":"https://www.appropedia.org/Appropedia:Copyrights","title":"CC-BY-SA-4.0"},"source":"''' Tafsiri '''\n\nAsali inaweza kusemwa kama kimiminika chenye ladha tamu ya sukari, chenye kunata na rangi ya manjano.\n\n== Matumizi ==\n\n=== Chakula ===\n\nAsali hutumika kama chakula, pia kama kiongezeo katika vyakula kama mkate, karanga na nafaka nyingine.\n\n=== Matibabu ===\n\nKatika sehemu nyingi duniani watu wanatumia asali katika kutibu magonjwa mbalimbali lakini pia katika kuongeza kinga ya mwili.\n\n== Lishe katika Asali ==\n\nAsali ni chanzo sahihi sana cha wanga kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na nishati.\n\n== Urinaji Asali ==\n\n=== Njia za jadi ===\n\nHistoria inaonesha urinaji asali umekuwapo kwa kipindi kirefu. Na njia ambazo zimekuwa zikitumika ni za jadi, kutoka na ubunifu asilia. Muhimu kufahamu njia hizi zimeendelea kutumika hadi sasa.\n\n=== Njia za kisasa ===\n\nNjia za kisasa zinazingatia utaalam katika kurina asali. Njia hizi huleta tija kutokana na kuzalisha asali kwa wingi katika eneo dogo.\n\n{{Page data\n| license = CC-BY-SA-3.0\n| language = sw\n}}\n\n[[Category:Food and agriculture]]"}