Tafsiri[edit | edit source]

Mazao ya biashara ni mazao yanayolimwa kwa dhumuni kuu la kuuzwa au biashara. Wakulima wengi hulima mazao haya wakiwa na nia ya kuyauza ni si kutumia wenyewe. Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa mbali na kulima mazao haya kwa nia kuu ya kuyauza, baadhi ya mazao haya hutumiwa na wakulima kwa matumizi yao ya kila siku kama vile chakula , nyenzo za kazi na matumizi maalum(vifaa vya ujenzi, dawa, vyakula vya mifugo n.k).

Mifano[edit | edit source]

Hapa ni muhimu kufahamu kuna mazao yanayoweza kutajwa kama mazao ya biashara na mazao ya chakula. Kwa mfano mahindi, maharagwe na mtama yanaweza kutajwa kama mazao ya biashara na pia mazao ya chakula. Hivyo basi mazao kama mahindi na mtama yanaweza kulimwa kwa ajili ya kuliwa na kaya husika ama kuuzwa. Mifano mingine ya mazao ya biashara ni kama vile mkonge, buni, pareto, chai, ufuta, alizeti, ngano na mengine mengi.


Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.