Upatikanaji wa maji salama ni muhimu katika kupigana na umaskini na matatizo ya afya. Watu maskini ambao wengi wao huishi vijijini wana nafasi finyu ya kupata maji safi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya mazao na matumizi ya afya. Faida za uchumi zinaweza kupatikana siyo kwa njia ya moja kwa moja tu bali kwa kuwa na afya bora na kuokoa muda unaotumika kuhangaika na kazi za kuchosha za kubeba maji kwa umbali mrefu. Takwimu zinaonyesha kuwa magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya maji hupatikana zaidi katika sehemu ambapo watu wanatumia maji yaliyoambukizwa au hawana maji ya kutosha kwa matumizi yao ya kila siku.

Idadi ya magonjwa hayo ni zaidi ya nusu ya magonjwa yanayowaathiri watu na kwamba asilimia themanini ya magonjwa yanayowashambulia watanzania wanaoishi vijijini

Yapi ni maji safi na salama?[edit | edit source]

Maji safi na salama ni maji yasiyokuwa na uchafu, yasiyo na harufu mbaya na yasiyo na vidudu. Maji safi na salama huleta afya njema na maji yasiyo safi na salama huleta madhara kwa binadamu kama vile kuhara na kuhara damu.

Ni vigumu na haiwezekani kutambua kwa macho kama maji ni safi na salama, hivyo ni muhimu kuchemsha maji kabla ya kuyatumia.

Usafi katika vyanzo vya maji[edit | edit source]

Njia sahihi za usafi katika vyanzo vya maji ni pamoja na kutumia visima vyenye mifuniko na kuhakikisha visima hivyo vinafunikwa baada ya kuteka maji. Kwa sababu kama majani na taka nyingine vitaanguka kisimani basi vitaoza na kuharibu maji. Pia ni vyema visima vichimbwe mbali kidogo na makazi ya watu. Hii ni kwa ajili ya kukilinda kisima dhidi ya taka za vyo na mazizi.

Njia zinazoweza kuchafua maji[edit | edit source]

Tabia kama vile kuoga, kufua nguo na kuchunga wanyama karibu na vyanzo vya maji kama vile maziwa, mito, mabwawa na visima huchafua maji sana. Kwa mfano wanyama wanaweza kuacha kinyesi katika maji.

Faharasa[edit | edit source]

Rivers-Smith, S. Afya, Macmillan and Co.,Ltd. London, 1966

Tovuti ya Taifa Tanzania

FA info icon.svg Angle down icon.svg Page data
Keywords food
Authors Christopher Sam
License CC-BY-SA-3.0
Language Kiswahili (sw)
Translations Kiingereza
Related 1 subpages, 1 pages link here
Impact 504 page views
Created Mei 20, 2011 by Christopher Sam
Modified Oktoba 23, 2023 by StandardWikitext bot
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.