Page data
Authors Christopher Sam
Published 2011
License CC-BY-SA-4.0
Impact Number of views to this page. Views by admins and bots are not counted. Multiple views during the same session are counted as one. 2,221

Maana[edit | edit source]

Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa ni magonjwa yanayoweza kuenezwa kwa kuvuta pumzi/hewa iliyo na vijidudu vya ugonjwa husika.

Mifano[edit | edit source]

Magonjwa yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya hewa ni kama vile surua, kifua kikuu (TB), n.k.

Surua[edit | edit source]

Ugonjwa wa surua hushambulia watu wa marika yote lakini hasa watoto chini ya miaka 5. Ni rahisi surua kuenea kwa watoto wenye afya duni ama magonjwa kama vile unyafuzi na nyongea. Surua inaua na hasa kama ikiambatana na magonjwa kama kutapika, kuharisha na vichomi. Pia surua inaweza kusababisha upofu(uthibitisho unahitajika).

Dalili[edit | edit source]

    • Kikohozi/Mafua
    • Macho mekundu
    • Homa kali, siku 3-4
    • Kuharisha/Kutapika
    • Vipele kinywani na baadaye mwili mzima.

Kinga[edit | edit source]

Kinga ya ugonjwa wa surua ni kwa njia ya chanjo, pia yapasa watoto wasiwe karibu ama kutokuchangia vitu na wagonjwa wa surua. Ukurasa huu ni kipisi tafadhali saidia kuendeleza!