WW-TLas200x200.gif
Project data
Completed 2011
OKH Manifest Open Know-How Manifest Download
Upload your project too!

Hii ni mbinu ya kuunga fito kwa kutumia makopo chakavu, kama makopo ya bati yaliyokwishatumika.

Vifaa unavyohitaji kuungia fito[edit | edit source]

WW PartsAndSize250.gif
 1. Fito mbili za kuunganishwa.
  • Hakikisha fito iko katika hali nzuri pale ambapo utaunganisha. Lazima iwe safi, kusiwe na vipande vya magome au rangi legevu na kusiwe na vidonda kwani sehemu hizi ni vigumu kupiga msumari.
 2. Vipande viwili vya bati jembamba.
  • Kwa kiungo cha kwanza.
  • Tumia kisu kukatia bati toka kopo dogo kwa mfano.
  • Urefu na upana sawa na kipenyo wa fito.
 3. Kipande kimoja cha metali ( sheet metal ).
  • Kwa kiungo cha mwisho.
  • Tumia ncha ya shoka au patasi kukata metali toka kwenye pipa la mafuta kwa mfano.
  • Kimo 3x ya kipenyo cha fito.
  • Urefu 6x ya kipenyo cha fito.
 4. misumari midogo, ~1 cm, kwa ajili ya kiungo cha kwanza.
 5. Misumari mikubwa, ~2.5 cm, kwa ajili ya kiungo cha mwisho.

Uungaji wa mpito[edit | edit source]

WW FirstBondStrip250.gif
 1. Amua sehemu nzuri kabisa kwa ajili ya fito hizo mbili.
 2. Unga pamoja, au uwe na mtu azishikilie fito katika sehemu zake.
 3. Tumia vipande viwili vya bati nyembamba na misumari midogo kutengeneza kiungo cha mpito katika pande zote mbili za fito kama ilivyooneshwa.
  • Usiweke mzigo kwenye sehemu za fito, tumia kiungo kuangalia kama kinafaa mipango yako tu.

Andaa mashimo madogo kwa ajili ya misumari ya 2.5 cm[edit | edit source]

WW PrepareHoles250.gif
 1. Tumia pini kali au msumari (~ 8cm) kutoboa matobo kwenye kipande cha metali
  • Yasiwe makubwa zaidi ya yanayohitajika na misumari. Vitobo vidogo unavyoweka baadae vitatoshea vichwa vya misumari, ndoana iliyo upande wa nyuma itatoa mshikilio wa ziada baadae itakapoingizwa ndani ya fito.
  • Toboa matundu karibuni na mwisho (0.5 cm) na yaachiane nafasi ya 2 cm.

Kuweka kipande cha metali kwenye kiungo[edit | edit source]

WW NailingStarts250.gif

Inahitaji uzoefu kufanya hili sawa, lakini kwa ujumla:

 1. Funika kiungo baina ya fito kwa kutumia kipande cha metali kwa kiasi kitakachoruhusu kona zake kukunjwa.
 2. Piga misumari mitatu kuunganisha kipande cha metali katika sehemu hiyo.

Kunja kona chini na zipigilie katika upande huu[edit | edit source]

WW NailingMore250.gif
In preparation.jpg

Baada ya kipande cha metali kuwekwa vizuri katika sehemu yake, unaweza:

 1. Kunja kona za kipand cha metali chini.
 2. Piga nyundo ncha za kipande cha metali kuzilaza dhidi ya fito.
 3. Pigilia misumari, upande huu wa kiungo.

Gonga nyundo kipande cha metali kuzungukia upande mwingine[edit | edit source]

WW NailingBending250.gif
 1. Nyanyua kiungo toka sakafuni na pindisha kipande cha metali juu hatua chache.
 2. Baada ya kila hatua ya kupindisha, gonga tena mwishoni mwa kipande cha metali ili ilale sambamba na fito.
 3. Iunganishe kwa kutumia msumari.
 4. Rudia hatua hizi mpaka kipande cha metali kizunguke kiungo.

Unganisha kipande cha metali katika mzunguko wote[edit | edit source]

WW NailingAround250.gif

Kiungo sasa kinajenga nguvu. Ongeza nguvu zaidi kwa kuchunguza ni vipi ncha zimelala dhidi ya fito. Kuliko na upenyo:

 1. Zifunge kwa kugonga kipande cha metali polepole kwa nyundo.
 2. Toboa kipande cha metali kwa pini kali.
 3. Ongeza msumari mwingine.
 4. Rudia kama ni lazima.
 5. Mwisho hakikisha hakuna vincha vya kipande cha metali au misumari vinavyotokeza nje. Kama vipo, Vigonge nyundo vilale, ili viungane na fito.
 6. Chunguza matokeo kwa kutembea vidole vyako kuzunguka kiungo. Inabidi uhisi ulaini katika mzunguko wote.

Hivi ni kama inavyoonekana baada ya kumaliza[edit | edit source]

WW ConnectionReady250.gif
mfano wa fito zilizoungwa katika matumizi
 • Kona za kipande cha metali lazima ziingiliane, zitengeneze duara na sio mnyongo.
 • Katika kona misumari inatoboa tabaka zote za kipande cha metali, kufunga mzunguko kwenye fito!
 • Kona tu zinaingiliana. Kama kipande cha metali ni kirefu sana, kata sehemu yake kusahihisha.
 • Mwisho chunguza tena kuona kwamba kiungo ni laini kwa nje, ili kisidake ngozi au nguo.
 • Kama haujaridhika, sahihisha au badilisha. Kuondoa:
  1. Bandua kipande cha metali kwa kutumia kisu au bisibisi.
  2. Vuta kipande cha metali toka kwenye fito kwa kutumia koleo. Kama utafanya kwa umakini, misumari itatoka wima kwa ajili ya kutumia tena.
  3. Gonga kipande cha metali kukinyoosha na anza upya. Kama ilivyo katika uchomaji vyuma, kuchoma fito kunahitaji mazoezi kufanya vyema.
Page data
Type Project
Keywords recycle, wood, welding, sheet metal, tin, how tos, wood working
SDG Sustainable Development Goal SDG11 Sustainable cities and communities
Published 2011
License CC-BY-SA-3.0
Language Kiswahili (sw)
Impact Number of views to this page and its redirects. Updated once a month. Views by admins and bots are not counted. Multiple views during the same session are counted as one. 173
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.