Get our free book (in Spanish or English) on rainwater now - To Catch the Rain.

Difference between revisions of "Kamusi la teknolojia"

From Appropedia
Jump to navigation Jump to search
(add "get involved" template)
Line 1: Line 1:
 +
{{KiswahiliGetInvolved}}
 
   This page is still in trial phase, but you are welcome to join forces!
 
   This page is still in trial phase, but you are welcome to join forces!
  

Revision as of 20:08, 19 March 2011

Jihusishe!
Appropedia ni wiki kwa hiyo unao uwezo wa kuhariri na kuchangia maelezo na kushirikiana na wengine kupunguza alama katika ikolojia yaani ecological footprint ili kuishi kitajiri na kindugu na mazingira yetu na maliasili. Unaweza kuanza kuchangia baada ya kutengeneza akaunti au ingia kama tayari unayo akaunti.
 This page is still in trial phase, but you are welcome to join forces!


Kamusi la teknolojia ni elezo huru litoalo tafsiri na maana ya meneno ya kiswahili katika nyanja ya teknolojia na pia maelezo kwa ufupi ya vifaa vya kiteknolojia. Kamusi la teknolojia likiwa ni elezo huru unakaribishwa kuongeza maarifa yako ama kuhariri maelezo yaliyomo ndani tayari. Changia sasa kuleta mabadiliko. Karibu!

Kapasita|kwa kiswahili(capacitor, in english). Kapasita ni kifaa kitumikacho kukusanya na kuhifadhi umeme. Katika muundo rahisi kabisa kapasita inaundwa na visahani viwili vya metali vinavyotenganishwa na maada isiyopitisha umeme, yaani daielektriki.

Uwezo wa kapasita kuhifadhi umeme ujulikana kama kapasitensi kifupisho ni C. Na kipimo chake katika mfumo wa kimataifa wa vipimo ni Faradi, kifupisho ni F. Lakini faradi 1 ni kubwa sana ivyo vipimo vidogo vya (1/1000)F=MFD, -1/1000000)F=NFD, (1/1000000000)F=PFD hutumika. Kimahesabu kiwango cha chaji kilichohifadhiwa na kapasita hupatikana kwa Q=CV, ambapo Q ni chaji, C ni kapasitensi na V ni volti. Kapasita ni kifaa muhimu sana katika vifaa vya elektroniki. Mbali na kuhifadhi umeme kapasita hutumika kusawazisha volti au mkondo wa umeme upitao. Pia kapasita hutumika kutambua mawimbi ya umeme, kama kwenye redio-kutafuta masafa ya redio mbalimbali.

Kipingizi, (w) vipingizi |kiswahili (in english resistor(s)). Kipingizi ni kifaa cha umeme kizuiacho au kipunguzacho kiasi cha mkondo wa umeme unaopita. Kama umeme utakuwa wa volti moja na kipingizi kikaruhusu mkondo wa umeme wa ampia moja, basi kipingizi kitakuwa na omu(ohm) moja. Katika sakiti ya umeme upingizi unaweza kutafutwa kimahesabu kwa R=V/I. Vipingizi vinapatikana katika viwango tofauti. Vilivyo katika maelfu huwekwa katika kilo omu na vilivyo katika mamilioni huwekwa katika mega omu.

Ampia |kiswahili (in english ampere). Ampia ni kipimo cha mfumo wa kimataifa cha vipimo cha kiasi cha mkondo wa umeme upitao katika sakiti. Kifupi chake ni A. Vifaa vingi vya umeme vya majumbani huwa vimeandikwa kiasi cha ampia zinazohitajika ili kifaa kiweze kufanya kazi. Kama mkondo utakuwa pungufu basi ni dhahiri kifaa kitashindwa kufanya kazi au kitafanya kazi lakini si kwa ufanisi. Na pengine hata kuharibika.

Tengeneza mwenyewe |kiswahili(in english do-it-yourself). Ni kitendo cha kutengeneza ama kukarabati vitu mbalimbali haswa vya nyumbani na matumizi binafsi mwenyewe badala ya kupeleka kwa fundi. Wengi hufanya tengeneza mwenyewe kutokana na mapenzi na wengine ni sehemu ya kuokoa gharama au kujifunza kwa vitendo. Kwa sasa kuna tovuti nyingi zenye miradi ya tengeneza mwenyewe.

Umeme mkondo mnyoofu |kiswahili(in english direct current).Umeme mkondo mnyoofu ni aina ya mkondo wa umeme ambao haubadili muelekeo. Hivyo katika graph umeme mkondo mnyoofu huoneshwa kwenye upande wa chanya tu. Vyanzo umeme mkondo mnyoofu ni pamoja na betri, umeme jua na umeme usio mkondo mnyoofu uliobadilishwa kuwa umeme mkondo mnyoofu. Umeme mkondo mnyoofu ndio aina ya umeme unaotumika kuendesha vifaa kama redio, simu za mikononi na baadhi ya mota. Lakini kutokana na ugumu wa kuuzidisha au kuupunguza umeme mkondo mnyoofu, umeme usio mkondo mnyoofu hutumika. Huu unaweza kuzidishwa au kupunguzwa kirahisi kabisa kwa kutumia transfoma.