We continue to develop resources related to the COVID-19 pandemic. See COVID-19 initiatives on Appropedia for more information.

Chakula

From Appropedia
Revision as of 10:59, 6 December 2011 by Kili (talk | Contributions)
(Difference) ← Older revision | Latest revision (Difference) | Newer revision → (Difference)
Jump to navigation Jump to search
Kiswahili - English

Maana[edit]

Chakula ni kitu ambacho watu ama wanyama wanakula na mimea inafyonza ili kuleta na kuwezesha uhai.

Hivyo chakula ni lishe. Afya bora inatokana na mpangilio mzuri wa ulaji wa chakula. Hapa ni muhimu kuzingatia uwiano mzuri wa makundi ya vyakula na muda wa milo.

Mara nyingi watu katika nchi zinazoendelea wanakumbwa na matatizo yanayosababishwa na ulaji wa chakula usiozingatia mpangilio ama uwiano mzuri wa makundi ya vyakula. Lakini hii inasababishwa na umaskini, njaa hasa inayosababishwa na hali mbaya ya hewa na ukame na miundombinu mibovu.

Katika nchi zinazoendelea watoto wengi na wazee wanaonekana kuwa na utapiamlo. Ukijionesha kupitia unyafuzi na kwashakoo.

Umuhimu wa chakula[edit]

Tunakula chakula ili kuondoa njaa na kuupa mwili virutubisho vya kuufanya uendelee kuwa na nguvu na afya bora. Chakula lazima kiwe safi na salama na kinatakiwa kiwe cha kutosha kulingana na umri, kazi na hali ya mtu. Ubora wa chakula pia hutegemea upatikanaji wa virutubisho vyote, yaani wanga, protini, mafuta, maji, madini na vitamini.

Madhara ya lishe duni[edit]

Madhara yafuatayo husababishwa na kutokuzingatia lishe bora.

 • Utapiamlo.
 • Kiriba tumbo.
 • Unyafuzi.
 • Kwashakoo.

Unyafuzi[edit]

Unyafuzi husababishwa na ukosefu wa virutubisho vya aina ya protini kama mayai, nyama n.k.

Dalili[edit]

 • Kupungua uzito.
 • Nywele za rangi ya shaba na dhaifu.
 • Tumbo kubwa.
 • Kuvimba kwa uso na miguu.
 • Kukosa hamu ya kula.

Nyongea[edit]

Nyongea husababishwa na kukosekana kwa wanga na mafuta ya kutosha katika chakula.

Dalili[edit]

 • Upungufu mkubwa wa uzito.
 • Kuzeeka kwa sura.
 • Kwa watoto hutaka kula wakati wote.
 • Macho meupe.

Kiribatumbo[edit]

Kiribatumbo husababishwa na kuzidi mafuta mwilini. Kiribatumbo huambatana na maradhi kama vile ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu.

Rovu[edit]

Rovu husababishwa na ukosefu wa madini joto/iodine mwilini. Rovu hujitokeza kwa kuvimba tezi za shingo. Pia kudumaa kwa akili na mwili hutokea.

Upungufu wa damu[edit]

Upungufu wa damu ama uwekundu wa damu husabisha udhaifu wa mwili, kuchoka mara kwa mara, kusinzia na kuhema haraka haraka. Tatizo hili usababishwa na upungufu wa madini chuma.

Kwashakoo[edit]

Kwashakoo husababishwa na ukosefu wa protini mwilini.

Dalili[edit]

 • Kuvimba tumbo.
 • Nywele laini zenye rangi ya shaba/nyekundu.
 • Ngozi mbaya iliyopasukapasuka.
 • Kuvimba kwa ini.
 • Upungufu wa damu.

Usomaji zaidi[edit]

http://en.wikipedia.org/wiki/Food

Ukurasa huu ni kipisi tafadhali saidia kuendeleza!