Kompyuta ni mashine ya kielekitroniki yenye uwezo wa kuhifadhi, kupanga, kutafuta na kupata maelezo, kukokotoa mahesabu na kusimamia mashine nyingine. Kompyuta pia zinatumika katika mawasiliano kupitia mtandao. Vilevile kompyuta ni mhimili mkubwa katika teknohama.