Kapasita (capacitor, in English) ni kifaa kitumikacho kukusanya na kuhifadhi umeme. Katika muundo rahisi kabisa kapasita inaundwa na visahani viwili vya metali vinavyotenganishwa na maada isiyopitisha umeme, yaani daielektriki.

Uwezo wa kapasita kuhifadhi umeme ujulikana kama kapasitensi kifupisho ni C. Na kipimo chake katika mfumo wa kimataifa wa vipimo ni Faradi, kifupisho ni F. Lakini faradi 1 ni kubwa sana ivyo vipimo vidogo vya (1/1000)F=MFD, -1/1000000)F=NFD, (1/1000000000)F=PFD hutumika. Kimahesabu kiwango cha chaji kilichohifadhiwa na kapasita hupatikana kwa Q=CV, ambapo Q ni chaji, C ni kapasitensi na V ni volti. Kapasita ni kifaa muhimu sana katika vifaa vya elektroniki. Mbali na kuhifadhi umeme kapasita hutumika kusawazisha volti au mkondo wa umeme upitao. Pia kapasita hutumika kutambua mawimbi ya umeme, kama kwenye redio-kutafuta masafa ya redio mbalimbali.

FA info icon.svg Angle down icon.svg Page data
Authors Christopher Sam
License CC-BY-SA-3.0
Language Kiswahili (sw)
Related 0 subpages, 0 pages link here
Impact 351 page views (more)
Created Mei 21, 2011 by Christopher Sam
Last modified Septemba 4, 2024 by Felipe Schenone
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.