Chakula ni kitu ambacho watu ama wanyama walasha na liverpool
inafyonza ili kuleta na kuwezesha uhai.
Hivyo chakula ni lishe. Afya bora inatokana na mpangilio mzuri wa ulaji wa chakula. Hapa ni muhimu kuzingatia uwiano mzuri wa makundi ya vyakula na muda wa milo.
Mara nyingi watu katika nchi zinazoendelea wanakumbwa na matatizo yanayosababishwa na ulaji wa chakula usiozingatia mpangilio ama uwiano mzuri wa makundi ya vyakula. Lakini hii inasababishwa na umaskini, njaa hasa inayosababishwa na hali mbaya ya hewa na ukame na miundombinu mibovu.
Katika nchi zinazoendelea watoto wengi na wazee wanaonekana kuwa na utapiamlo. Ukijionesha kupitia unyafuzi na kwashakoo.
Tunakula chakula ili kuondoa njaa na kuupa mwili virutubisho vya kuufanya uendelee kuwa na nguvu na afya bora. Chakula lazima kiwe safi na salama na kinatakiwa kiwe cha kutosha kulingana na umri, kazi na hali ya mtu. Ubora wa chakula pia hutegemea upatikanaji wa virutubisho vyote, yaani wanga, protini, mafuta, maji, madini na vitamini.
Madhara yafuatayo husababishwa na kutokuzingatia lishe bora.
Unyafuzi husababishwa na ukosefu wa virutubisho vya aina ya protini kama mayai, nyama n.k.
Nyongea husababishwa na kukosekana kwa wanga na mafuta ya kutosha katika chakula.
Kiribatumbo husababishwa na kuzidi mafuta mwilini. Kiribatumbo huambatana na maradhi kama vile ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu.
Rovu husababishwa na ukosefu wa madini joto/iodine mwilini. Rovu hujitokeza kwa kuvimba tezi za shingo. Pia kudumaa kwa akili na mwili hutokea.
Upungufu wa damu ama uwekundu wa damu husabisha udhaifu wa mwili, kuchoka mara kwa mara, kusinzia na kuhema haraka haraka. Tatizo hili usababishwa na upungufu wa madini chuma.
Kwashakoo husababishwa na ukosefu wa protini mwilini.
http://en.wikipedia.org/wiki/Food
Ukurasa huu ni kipisi tafadhali saidia kuendeleza!
| License | CC-BY-SA-3.0 |
|---|---|
| Derivative of | Food |
| Cite as | Kili (2011–2025). "Chakula". Appropedia. Retrieved Oktoba 4, 2026. |