FA info icon.svg Angle down icon.svg Organization data
Founded 2003
Founders Mitra Ardron
Location Australia
Site naturalinnovation.org/
Green hosting No

Natural Innovation ilianzishwa mwaka 2003 kuwezesha uendelezaji wa teknolojia safi, na imekuwa na mafanikio makubwa katika nyanja za vifaa kutoka taka, kilimo cha mjini na umeme jua.

Mwishoni mwa mwaka 2009 tuligundua kwamba mawazo mengi mazuri ambayo yangekuwa na tija katika kupunguza hewa za sumu na umaskini yamekuwa yakipotea kutokana na changamoto za kifedha. Tulihisi kuna njia zingine za kunyanyua uwezeshaji wa wazo linalosadifu hali ya mtaji wa kienyeji au sehemu husika, na hasa kama wabunifu wana chachu ya kutoa kwa dunia na sio kutengeneza hela.

Mara nyingi watu wanatujia pale wanapokuwa na wazo na wametumia muda wa kutosha, na mara nyingi pia hela, wakijaribu kuendeleza mawazo yao katika njia mbalimbali. Katika hatua hii ubunifu mwingi unaweza kupata mtaji, lakini hii inaweza kuwa ngumu kama wazo haliwezi kusajiliwa (kwa mfano kama limekwisha chapwa), au kama watu watakaonunua ubunifu ni maskini, au kwa kuwa wabunifu wako mbali na mabepari/wenye mtaji walio tayari kufanyia kazi ubunifu husika.

Nini[edit | edit source]

Tunawaleta pamoja innovators, engineers & na wengine wanaojitoleao, philanthropists & foundations, wakopeshaji kama taasisi za mikopo midogo, na asasi za maendeleo na misaada. Tunawasaidia wabunifu kufikia rasilimali wanazohitaji kuhakikisha ubunifu wao unakamilika kisha unawafikia watu wanaouhitaji. Tutasaidia kuondoa hatari ya hasara katika ubunifu – kuunda bidhaa ya kwanza kwa mfano, au kujaribu soko, ili vyanzo nafuu vya uwezeshaji kifedha, au wabia husika zaidi katika hatari ya hasara (kama asasi za misaada) waweze kusaidia usambazaji.

Wabunifu[edit | edit source]

Natural Innovation Foundation inafanya kazi na wabunifu wenye mawazo mazuri yanayoonekana kuwa na tija na uwezekano wa kuwekwa katika skeli na pia uwezo wa kuondoa umaskini au uboreshaji mazingira. Ubunifu mwingi tunaofanyia kazi unatilia mkazo kwenye nchi zinazoendelea, na wengi wa wabunifu wako.

Tunafanya kazi na wabunifu hawa kuwasaidia kutekeleza mawazo yao kwa kuondoa hatari ya hasara (kwa mfano kutengeneza bidhaa ya kwanza, au kujaribu soko) na kuskeli (scaling).

Tunawaonganisha wabunifu na rasilimali – hii ikjumuisha misaada; wanaojitolea (hasa kiufundi); mikopo na wabia/mapatna husika.

Tovuti rasmi:http://www.naturalinnovation.org/

FA info icon.svg Angle down icon.svg Page data
Keywords innovation, australian organizations, international organizations
Authors Christopher Sam
License CC-BY-SA-3.0
Derivative of Natural Innovation
Language Kiswahili (sw)
Related 0 subpages, 1 pages link here
Impact 404 page views
Created Aprili 11, 2011 by Christopher Sam
Modified Oktoba 23, 2023 by Maintenance script
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.