Template:Lang

Presstwo.JPG

Maelezo

Mradi huu ni uchunguzi wa matofali ya udongo uliogandamizwa. Sababu kubwa ni mazuri sana.

Fursa

CCAT, the campus center for appropriate technology, punde hii imehama na maeneo yake mapya mengi yana vilima ambavyo bado havijadhibitiwa. Kuna matatizo ya mmomonyoko wa udongo na majanga yanayosababishwa na maji toka milimani juu ya udongo mfinyanzi, hitaji la kingo za kuta za kuzuia ni la haraka.

Marejeo/Fasihi

Mambo makuu juu ya Matofali ya Udongo Uliogandamizwa

Matofali ya Udongo Uliogandamizwa ni matofali ya kujengea yaliyotengenezwa kwa ulioimarishwa au usioimarishwa na kugandamizwa. Mgandamizo upo kuanzia mamia ya paundi mpaka tani kadhaa. Kwasababu ya hali kubwa ya kudumu inayopatikana matofali yasiyoimarishwa yanatumika pale tu ambako hakuna kitu cha kuimarisha matofali hayo. Zaidi ya kuimarisha, matofali haya ya udongo yanatengenezwa kwa ajili ya kudumu, urahisi wa kazi/kuyatumia, na muda wa kuishi na kuimili hali mbalimbali za hewa.

Tofali linapogandamizwa linapoteza asilimia 30 ya ujazo wake. Hii ni kutokana na mgandamizo wa kimakanika wa presi inayoondoa vifuko vya hewa na kupanga chembe za udongo mfinyanzi na kuzigandamiza pamoja kuzunguka chembe za mchanga.[1]


Uimarishaji

Kuna vitu vingi sana vinaweza kutumika kwa ajili ya kuimarisha. Kwa ujumla vinaweza vikapangwa katika vile vya asili na vile toka viwandani. Vinajumuisha vitu kama vile juisi za mimea, mabaki ya maziwa wakati wa kutengeneza siagi, utomvu, mabaki ya miwa/molasesi, majivu ya kuni, na chokaa kutaja vichache. Hapa Marekani, kutokana na kuwepo kwa saruji ya gharama nafuu inaongeza ufanisi wa kifizikia na kiuchumi kuitumia[1][2]. Baadhi ya vyanzo havishauri kutumia vitu vya kuimarisha tofauti na saruji hata kama unajenga katika nchi zinazoendelea[3]


Karatasi kama kiimarisho Pepakriti, bidhaa ya karatasi na saruji ya kujengea, imetafitiwa sana na kujaribiwaa.[2] Karatasi zilizopo katika pepakriti inadhaniwa kusababisha matokeo mazuri kama kiimarishaji. Matatizo yanayoambatana na pepakriti ni pamoja na uvundo(mold?), kusinyaa na kukauka polepole.[3] [1]

Vigezo

kigezo binafsi mradi umebadilishwa mafanikio
Kazi ya timu/ushirikiano 7 7 51%
Uendelevu 7 7 99%
Majaribio 10 10 92%
Matofali ya bidhaa 2 6 49%
Bajeti 4 1 82%
kujirudia 10 10 84%
Elimu 10 10 100%

Mwishoni, utaratibu ukashinda dhidi ya bidhaa. Dazeni tatu tu za matofali zimetengenezwa mpaka sasa. Kwa kusema hayo, nina furaha sana juu ya uzoefu na malengo ya msingi, elimu, majaribio,na uwezo wa kujirudia, ambavyo vimeweza kufikiwa.

Gharama

vitu gharama
Mchanga (kwa uzuni baada ya maamuzi ya mwisho juu ya mchanga uliopo sehemu ya tukio/saiti =(umenunuliwa) 30$
Saruji 45$
Boric Acid(as ortho boric acid from coachroach poison) 6$
Trashcan(longlife) 30$
Mbao laini 30$
Reki(2) 30$
Chepe 20$
glovu 10$
Kifaa cha kuhifadhia 130$
JUMLA (kadirio) 315$

Maandalizi

Upimijai wa udongo:

Baada ya kupima udongo wako, vizuri sehemu tofauti tofauti, utakuwa na mchanganyiko ambao una asilimia 75 mchanga na angalau asilimia 10 mfinyanzi na pungufu ya asilimia 35 mfinyanzi kwa ujazo.[1] Kiwango cha saruji kitahusiana na jinsi gani umekaribia viwango hivi, Kati ya 3-5% mpaka 10%.[1]. Sasa kufikiria juu ya kutengeneza matofali ya udongo uliogandamizwa...

Kupima udongo:

Baada ua kusoma majaribio yote, kama 6 yanatumika sana kwa sasa, nilichagua mawili ambayo ni rahisi kupita yote. Nilichagua ‘jaribio la bloku’ na ‘jaribio la maji ya chumvi’.

Jaribio la bloku:

Jaribio la bloku katika hali rahisi, ni kutengeneza bloku lako toka katika udongo na kupima kusinyaa. Hii inahitaji ish box ndefu, fikiria zaidi ya futi 4 kwa inchi 4. Kuta za boksi lazima ziwe zinateleza la sivyo mafuta yatumike.
Majaribio matatu ya bloku, kusinyaa kabla

Jaribio la maji ya chumvi:

Kufanya jaribi hili: ongeza chumvi na maji kwa angalau kikombe cha udongo katika chombo kinachoonesha. Tumia kijiko cha chai kwa kikombe cha udongo na funika udongo na maji. tikisa. Kisha acha utulie kwa muda wa nusu saa hivi. Angalia na pima kiwango cha mnyumbuliko wa udongo.

Kama ifuatavyo:


Fig 1:chombo kinachoonesha na maji
Fig 2:weka udongo, tikisa na acha utulie
File:CCAT cebs Separation-test.jpg
Fig 3: pima


Dibaji ya matumizi ya Ram:

Hii ni kazi ya kikundi kinadharia. Kiwango cha chini cha watu wanaohitajika ni wawili kuweza kutumia mashine ya CINVA-ram. Watu wane vizuri, sita wanafaa zaidi kutokana na uzoefu wangu. Nitaeleza kwa kifupi juu ya mashine isiyo ya kimakanika inayohitaji kujitoa na vifaa vichache.

Vitu vinavyohitajika(kwa uchanganyaji usio wa kimakanika):

  • reki ya chuma
  • ndoo kadhaa(1-3)
  • sehemu ya kuchanganyia(kipande cha ubao, kama kipo, kuepuka kuchanganya na saruji katika udongo)
  • maka
  • chepe
  • vipimo (rula, tape measure, fimbo, n.k.)

Utahitaji kujua mchanganyiko wako kulingana na ndoo zako. Kama unachanganya udongo wako na mfinyanzi au mchanga itabidi utumia njia nilizotumia kupata vipimo vya wastani ili kupata viwango vya saruji.

Tambua mchanganyanyiko wako

Kwanza, jaza ndoo kwa mchanganyiko wa udongo, kisha weka kwenye sehemu ya kuchanganyania. Jaza ndoo tena, lakini nusu, na kisha tumia maka kuweka alama nusu kuzunguka ndoo, mstari wa lebo. Kwa hivyo weka lebo kila kitu. Hii ni kazi ya kikundi kwa hiyo lebo zitasiadia kuepuka kuchanganyana na kukosea. Weka ndoo ya pili katika sehemu ya kuchanganyia, weka kifusi kimoja, gawanya kifusi hiki katika sehemu kumi zinazolingana. Hii itahitaji kazi kidogo, usijaribu kuwa bila makosa kabisa, fanya kazi nzuri na endelea. Kwa umakini weka kifusi kimojawapo katika ndoo, weka alama ndogo ndani ya ndoo kuweka alama ya mahli ulipofikia udongo. Rudia utaratibu huu mara mbili zaidi. Kadiria sehemu ulizo weka alama. Sasa chora mstari, sehemu ya umbali uliopimwa toka sehemu nusu ya mstari wako. Lebo mstari huu mpya, ambao utakuwa umbali mdogo toka nusu ya mstari wako, ‘saruji’. Hii inakupa walau asilimia kumi ya saruji ya kuimarisha wakati wa kupima. Kama unapima kupata mchanganyiko mzuri, badilisha kiwango cha saruji toka asilimia 10 mpaka asilimia 5 kwa kufanya nusu umbali wa mistari ya saruji na udongo. Kisha kufanywa nusu tena kati ya asilimia 5 za jaribio mpaka asilimia. Baadhi ya ponti katika maandiko zinaoonesha kiwango cha saruji kufikia hadi asilimia 2. Lakini kama unatumia kiimiarishaji kingine utahitajika kutumia mara mbili zaidi.

Sasa haswa namna ya kutengeneza matofali ya udongo uliogandamizwa...

Mradi

Nilijaribu kutumia mpango wa zamani wa "workshop = group labor camp" kwa mafanikio kidogo. Kundi langu la mafanikio zaidi likawa darasa la uhandisi 305. Amini kwamba wamarekani wengi sio wazuri katika kazi za nguvu tena. Maandiko yanaeleza kwamba CINV-ram iliyotumika, ambayo imetengenezw Bogotá, Colombia, inaweza kuzalisha kati ya matofali 40 mpaka 60 kwa saar[1]. matokeo mazuri kabisa tuliyomudu ni robot u kwa timu ya watu 14.


Kazi Idadi ya watu
Kuchimba 4 3 2 2 1 1 1
Kusafirisha 3 2 2
Kupima na kujaribu 1 2 2 2 1
Kuchanganya 2
Kujaza na kusawazisha 1 1 1
Kugandamiza 1 1 2 1 1
kutokeza nje 1 1
Kutoa na kukausha 2 1
Jumla ya nguvu watu 15 10 8 6 3 2



Kazi ya timu inamaanisha kuwa na muendelezo mzuri (Angalia jedwali hapo juu) ya:

kuchimba kuchukua udongo toka sehemu nzuri, kutenganisha bila umakini, kuchukua mawe na vitu vya mimea.
Kuhamisha kusafirisha udongo toka sehemu ulikopatikana kwenda saiti.
Kutenganisha kujaza ndoo katika mistari sahihi.
Kuchanganya kusambaza saruji sehemu zote, au kiimarishaji kingine, kwa udongo wote uliobaki.
Kujaribu kuangusha mchanganyiko kwa kujaribu ili kuhakikisha kiwango sahihi cha unyevunyevu, kuongeza maji kama inavyolazimu.
Kujaza kujaza sehemu wazi katika gandamizo, kuacha gandamizo safi.
kugandamiza kuendesha nyenzo za gandamizo kugandamiza tofali.
Kuachia kuendesha nyenzo za gandamizo kuachia tofali. Kutoa na kusafirisha – kutoa tofali katika gandamizo na kupeleka katika eneo la kuhifadhia.
kupanga kupanga matofali na kuweka pembeni matofali yaliyobomoka kwa ajili ya kutengenezwa tena.


Muendelezo mzuri unahitaji kuasili. Kazi zinaingiliana, vikwazo vinatokea, watu wanachoka, mawasiliano na urahisi wa kubadilika kwa kazi ya kila mmoja ni vitu vinavyoweza kuunda mfumo mzuri wa kazi ya timu, kitu kinachofurahisha siku zote.


Kuendesha gandamizo ni kama ifuatavyo


changanya vizuri Kazi ya timu inafurahisha While working, it is best to practice your bigfoot pose as much as possible
Combobulate.JPG
Teamworkmakessmiles.JPG
Teamworkis.JPG


Na kumbuka kumwagilia matofali yako! Saruji inachukua wiki kadhaa kama sio miezi kukamilika. Kadirio la chini loanisha kwa wiki.

Majaribio

Matofali yaliyogandamizwa ya karatasi niliyotengeneza bado yanakauka, nitayaweka katika hali ya kulowana(saruji ikomae) na nitayajaribu baada ya mwezi. Kwa kusema hayo, karatasi ilifanya matofali kuwa imara zaidi toka katika gandamizo. Kutayarisha karatasi kwa ajili ya kuchanganya ilikuwa kazi sana. Nilitumia dumu la plastiki kuhifadhia karatasi katika maji.


Niliongeza boric acid katika mchanganyiko wa galoni 50 za maji na karatasi kuzuia kuvunda(molding?). kuvunda kunatajwa sana kama tatizo la pepakriti (bidhaa inayokaribiana sana na ninachojaribu)[4]. Lakini, boric acid inaweza kutumika katika kuzuia uvundo.[5]. mchanganyiko wangu wa karatasi/maji/boric acid umekuwa rahisi kutunza na hauna uvundo kwa wiki sita mpaka sasa.

kuweka ortho boric acid
acha maji yatoke kidogo
hii inaweza kuwa njia nzuri kuliko...


Nilisaga karatasi zilizokuwa katika maji baada ya wiki kwa kutumia drili iliyowekwa kisu cha kuchanganyia. Baadae tena baada ya wiki moja. Nikweka juu ya skrini ikauke.


Baada ya kukauka nikaweka katika ndoo na nikatumia drili kupunguza ukubwa wa chembechembe. Utaratibu huu unamafanikio kidogo naweza kusema. Muda mwingi kupitiliza unwekezwa, na tokeo la mwisho halikuwa na chembechembe ndogo kutosha kutawanishwa sawia.

Majadiliano

Huu ni uchunguzi usio wa kina kuhusu matofali ya udongo uliogandamizwa. Hii teknolojia imetawaliwa na viwanda na faharasa zangu ni za muongo au muda zaidi uliopita.

Hali kuwa mchakato huu ni wa kiutunzaji, unachukua muda na nguvu kazi kwa kiasi kikubwa.

My interest in new materials that are 'hyper' efficient is ever persistent, feel free to contact me with questions and comments. eghant atgmail d0tc0m

Faharasa

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Stulz, Roland, and Kiran Mukerji. Appropriate Bulding Materials. 3rd ed. UK: Swiss Centre for Development Cooperation in TEchnology and Management, 1993.
  2. Spense, R.j.s., and D.j. Cook. Building Materials in Developing Countries. New York: John Wiley and Sons, 1983.
  3. Crystal.Netbook. Federal Ministry for Economic Cooperation and Development. http://www.crystal-netbook.info/

Angalia pia

Template:Attrib class

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.