Maji safi

Revision as of 10:32, 20 May 2011 by Kili (Talk | Contributions) (Created page with "==Yapi ni maji safi na salama?== Maji safi na salama ni maji yasiyokuwa na uchafu, yasiyo na harufu mbaya na yasiyo na vidudu. Maji safi na salama huleta afya njema na maji yasiy...")

(Difference) ← Older revision | Latest revision (Difference) | Newer revision → (Difference)

Yapi ni maji safi na salama?

Maji safi na salama ni maji yasiyokuwa na uchafu, yasiyo na harufu mbaya na yasiyo na vidudu. Maji safi na salama huleta afya njema na maji yasiyo safi na salama huleta madhara kwa binadamu kama vile kuhara na kuhara damu.

Ni vigumu na haiwezekani kutambua kwa macho kama maji ni safi na salama, hivyo ni muhimu kuchemsha maji kabla ya kuyatumia.

Usafi katika vyanzo vya maji

Njia sahihi za usafi katika vyanzo vya maji ni pamoja na kutumia visima vyenye mifuniko na kuhakikisha visima hivyo vinafunikwa baada ya kuteka maji. Kwa sababu kama majani na taka nyingine vitaanguka kisimani basi vitaoza na kuharibu maji. Pia ni vyema visima vichimbwe mbali kidogo na makazi ya watu. Hii ni kwa ajili ya kukilinda kisima dhidi ya taka za vyo na mazizi.

Njia zinazoweza kuchafua maji

Tabia kama vile kuoga, kufua nguo na kuchunga wanyama karibu na vyanzo vya maji kama vile maziwa, mito, mabwawa na visima huchafua maji sana. Kwa mfano wanyama wanaweza kuacha kinyesi katika maji.

References

Rivers-Smith, S. Afya, Macmillan and Co.,Ltd. London, 1966