The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.

Kitabu hiki ni kwa niaba ya Wizara ya Kilimo Tanzania na kinapatikana hapa

MWENDELEZO NAMNA YA KULIMA TANGAWIZI


KILIMO BORA CHA TANGAWIZI


Tangawizi ni moja kati ya aina za mazao ya viungo ambayo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Zao hili kwa lugha ya kigeni linafahamika kama Zingiber officinale.

UDONGO NA KUSTAWI

Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha milimita 1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi joto 20°C-25°C. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usio-tuamisha maji.

AINA

Mpaka hivi sasa hakuna aina rasmi za tangawizi ambazo zimeainishwa na kuthibitishwa kuzalishwa nchini Tanzania. Pamoja na hili, kuna aina tatu za tangawizi ambazo zimezoeleka kuzalishwa na wakulima hapa nchini. Aina hizo ni Tangawizi nyeupe maarufu kama White Africa au Jamaica, Cochin (flint), na Bombay.

Tangawizi inayopandwa katika sehemu tambarare huwa laini zaidi kuliko inayozalishwa kwenye maeneo ya milima, ambayo huwa ngumu na kuwa na nyuzi nyingi zaidi.

NAFASI

Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita 23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita 5-10. Unaweza kupanda sehemu yenye miti au migomba ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji mara kwa mara endapo mvua inakosekana hadi kufikia mwezi mmoja kabla ya kuvuna.

MATUMIZI

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji kama vile chai, soda, juisi, vilevi na kadha-lika. Kuna aina mbalimbali za vyakula ambavyo pia hutengenezwa kwa kutumia tangawizi kama vile mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari na kadhalika.

Tangawizi pia hutumika katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi. Hali kadhalika tangawizi hutumika katika kutengeneza vipodozi vya aina mbalimbali vile kama poda

MBEGU NA NAMNA YA KUPANDA

Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu. Vipande vya tangawizi huhifadhiwa mahali pakavu penye ubaridi ili kuweza kuchipua.

Machipukizi hukatwa urefu wa sen-timita 2.5-5. Baada ya hapo, unaweza kupanda machipukizi hayo kwenye matuta au shambani kawaida endapo eneo lako ni tambarare.

Baada ya kupanda, tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.

MATAYARISHO

Ondoa takataka zisizohitajika shambani. Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekari moja.

PALIZI

Katika kipindi cha wiki mbili, magugu huanza kuchomoza kwa kuwa udongo huwa na unyevu kwa wingi. Fanya palizi mara majani yanapojitokeza.

Endelea kung’oa magugu na kuweka shamba katika hali ya usafi hadi wakatiwa kuvuna.

KUPANDA

Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futimbili na majani yake ni membamba marefu, ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.

MAGONJWA NA WADUDU

Madoa ya majani: Yanayosababishwa na viini vya magonjwa viit- wavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.

Kuoza kwa tunguu: Kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp. Mizizi fundo: Inasababishwa na Meloidegyne spp.

UVUNAJI

Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapo-geuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa.

Tangawizi itakayohifad-hiwa ivunwe mapema kabla haijako-maa kabisa, na ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana kwa hekari moja.

SOKO LA TANGAWIZI


Soko la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, kiasi kikubwa kinauzwa nchini. Bei yake ni kati sh. 300-1,500/- kwa kilo moja kutegemeana na msimu.

FA info icon.svg Angle down icon.svg Page data
License CC-BY-SA-3.0
Language Kiswahili (sw)
Related 0 subpages, 0 pages link here
Impact 789 page views
Created Oktoba 8, 2011 by Christopher Sam
Modified Novemba 15, 2022 by Felipe Schenone
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.