(add "get involved" template)
No edit summary
Line 17: Line 17:


'''Umeme mkondo mnyoofu''' |kiswahili(in english direct current).Umeme mkondo mnyoofu ni aina ya mkondo wa umeme ambao haubadili muelekeo. Hivyo katika graph umeme mkondo mnyoofu huoneshwa kwenye upande wa chanya tu. Vyanzo umeme mkondo mnyoofu ni pamoja na betri, umeme jua na umeme usio mkondo mnyoofu uliobadilishwa kuwa umeme mkondo mnyoofu. Umeme mkondo mnyoofu ndio aina ya umeme unaotumika kuendesha vifaa kama redio, simu za mikononi na baadhi ya mota. Lakini kutokana na ugumu wa kuuzidisha au kuupunguza umeme mkondo mnyoofu, umeme usio mkondo mnyoofu hutumika. Huu unaweza kuzidishwa au kupunguzwa kirahisi kabisa kwa kutumia transfoma.
'''Umeme mkondo mnyoofu''' |kiswahili(in english direct current).Umeme mkondo mnyoofu ni aina ya mkondo wa umeme ambao haubadili muelekeo. Hivyo katika graph umeme mkondo mnyoofu huoneshwa kwenye upande wa chanya tu. Vyanzo umeme mkondo mnyoofu ni pamoja na betri, umeme jua na umeme usio mkondo mnyoofu uliobadilishwa kuwa umeme mkondo mnyoofu. Umeme mkondo mnyoofu ndio aina ya umeme unaotumika kuendesha vifaa kama redio, simu za mikononi na baadhi ya mota. Lakini kutokana na ugumu wa kuuzidisha au kuupunguza umeme mkondo mnyoofu, umeme usio mkondo mnyoofu hutumika. Huu unaweza kuzidishwa au kupunguzwa kirahisi kabisa kwa kutumia transfoma.
'''Dayaoda''' ni kifaa cha kielektroniki kipitichasho mkondo wa [[umeme]] kwenda upande mmoja tu kwa urahisi na kwa ugumu sana kwenda upande mwingine. Kuna aina mbalimbali za dayoda kama vile [[zena dayoda]], [[schottky dayoda]] n.k, zote zikiwa na kazi maalum ingawaje kuna muda zinaweza kuingiliana. Kutokana na tabia hii dayoda hutumika katika kubadilsiha umeme usio mkondo mnyoofu kwenda katika umeme mkondo mnyoofu.
'''Inveta''' ni kifaa kitumikacho kubadilisha umeme mkondo mnyoofu kwenda katika umeme usio mkondo mnyoofu. Hii inafanyika ili kuweza kutumia umeme kirahisi katika vifaa vya umeme ambavyo vingi vinatumia [[umeme]] usio mkondo mnyoofu, yaani a.c. Baada ya umeme kubadilishwa basi unaweza kupoozwa ama kupaishwa kirahisi kwa kutumia [[transfoma]] , hili haliwezi kufanyika katika umeme mkondo mnyoofu. Ni muhimu kutambua kwamba katika ubadilishaji kiasi cha nusu ya umeme kinapotea na kwa kuwa inveta haina ufanisi wa asilimia mia moja.
'''Voltimita''' ni kifaa kinachotumika kupima volti katika sakiti ya [[umeme]]. Ili kupima volti, voltimita huwekwa sambamba na sehemu ama chombo kinachoitajika kupimwa volti zake. Volti zinaweza kuweka katika moja ya elfu moja, yaani mV, moja mara, yaani 1×V, 10×V n.k. Lakini katika siku za usoni voltimita zinashindwa umaarufu na maltimita na zinaanza kupotea ama kupatikana kwa shida. Hii ni kwa sababu maltimita inafanya kazi nyingi zaidi, kwa mfano kupima kiasi cha mkondo wa umeme, kapasitensi na volti.
'''Kinuupepo''' ni mashine ya kufua umeme kwa kutumia msukumo wa upepo. Hapo zamani, vinuupepo vya kwanza vilikuwa vikitumika katika usagaji wa nafaka na pia kuendesha pampu za kufyonza maji na kukausha maeneo yasiyo makavu. Katika siku za usoni vinuupepo vimekuwa maarufu sana kutokana na kuzalisha nishati hai ya [[umeme]]. Hii inasaidi kupunguza [[alama ya hewa ya ukaa]]. Kinuupepo cha kufua umeme kinajumuisha mapanga yanayozungushwa na upepo ambayo huzungusha kwanza giaboksi kasha giaboksi huzungusha jenereta. Mzunguko huu huzalisha mkondo wa umeme. Umaarufu mkubwa wa vinuupepo umekuja kutokana na msukumo kuelekea [[nishati hai]].

Revision as of 08:31, 20 April 2011

Template:KiswahiliGetInvolved

 This page is still in trial phase, but you are welcome to join forces!


Kamusi la teknolojia ni elezo huru litoalo tafsiri na maana ya meneno ya kiswahili katika nyanja ya teknolojia na pia maelezo kwa ufupi ya vifaa vya kiteknolojia. Kamusi la teknolojia likiwa ni elezo huru unakaribishwa kuongeza maarifa yako ama kuhariri maelezo yaliyomo ndani tayari. Changia sasa kuleta mabadiliko. Karibu!

Kapasita|kwa kiswahili(capacitor, in english). Kapasita ni kifaa kitumikacho kukusanya na kuhifadhi umeme. Katika muundo rahisi kabisa kapasita inaundwa na visahani viwili vya metali vinavyotenganishwa na maada isiyopitisha umeme, yaani daielektriki.

Uwezo wa kapasita kuhifadhi umeme ujulikana kama kapasitensi kifupisho ni C. Na kipimo chake katika mfumo wa kimataifa wa vipimo ni Faradi, kifupisho ni F. Lakini faradi 1 ni kubwa sana ivyo vipimo vidogo vya (1/1000)F=MFD, -1/1000000)F=NFD, (1/1000000000)F=PFD hutumika. Kimahesabu kiwango cha chaji kilichohifadhiwa na kapasita hupatikana kwa Q=CV, ambapo Q ni chaji, C ni kapasitensi na V ni volti. Kapasita ni kifaa muhimu sana katika vifaa vya elektroniki. Mbali na kuhifadhi umeme kapasita hutumika kusawazisha volti au mkondo wa umeme upitao. Pia kapasita hutumika kutambua mawimbi ya umeme, kama kwenye redio-kutafuta masafa ya redio mbalimbali.

Kipingizi, (w) vipingizi |kiswahili (in english resistor(s)). Kipingizi ni kifaa cha umeme kizuiacho au kipunguzacho kiasi cha mkondo wa umeme unaopita. Kama umeme utakuwa wa volti moja na kipingizi kikaruhusu mkondo wa umeme wa ampia moja, basi kipingizi kitakuwa na omu(ohm) moja. Katika sakiti ya umeme upingizi unaweza kutafutwa kimahesabu kwa R=V/I. Vipingizi vinapatikana katika viwango tofauti. Vilivyo katika maelfu huwekwa katika kilo omu na vilivyo katika mamilioni huwekwa katika mega omu.

Ampia |kiswahili (in english ampere). Ampia ni kipimo cha mfumo wa kimataifa cha vipimo cha kiasi cha mkondo wa umeme upitao katika sakiti. Kifupi chake ni A. Vifaa vingi vya umeme vya majumbani huwa vimeandikwa kiasi cha ampia zinazohitajika ili kifaa kiweze kufanya kazi. Kama mkondo utakuwa pungufu basi ni dhahiri kifaa kitashindwa kufanya kazi au kitafanya kazi lakini si kwa ufanisi. Na pengine hata kuharibika.

Tengeneza mwenyewe |kiswahili(in english do-it-yourself). Ni kitendo cha kutengeneza ama kukarabati vitu mbalimbali haswa vya nyumbani na matumizi binafsi mwenyewe badala ya kupeleka kwa fundi. Wengi hufanya tengeneza mwenyewe kutokana na mapenzi na wengine ni sehemu ya kuokoa gharama au kujifunza kwa vitendo. Kwa sasa kuna tovuti nyingi zenye miradi ya tengeneza mwenyewe.

Umeme mkondo mnyoofu |kiswahili(in english direct current).Umeme mkondo mnyoofu ni aina ya mkondo wa umeme ambao haubadili muelekeo. Hivyo katika graph umeme mkondo mnyoofu huoneshwa kwenye upande wa chanya tu. Vyanzo umeme mkondo mnyoofu ni pamoja na betri, umeme jua na umeme usio mkondo mnyoofu uliobadilishwa kuwa umeme mkondo mnyoofu. Umeme mkondo mnyoofu ndio aina ya umeme unaotumika kuendesha vifaa kama redio, simu za mikononi na baadhi ya mota. Lakini kutokana na ugumu wa kuuzidisha au kuupunguza umeme mkondo mnyoofu, umeme usio mkondo mnyoofu hutumika. Huu unaweza kuzidishwa au kupunguzwa kirahisi kabisa kwa kutumia transfoma.

Dayaoda ni kifaa cha kielektroniki kipitichasho mkondo wa umeme kwenda upande mmoja tu kwa urahisi na kwa ugumu sana kwenda upande mwingine. Kuna aina mbalimbali za dayoda kama vile zena dayoda, schottky dayoda n.k, zote zikiwa na kazi maalum ingawaje kuna muda zinaweza kuingiliana. Kutokana na tabia hii dayoda hutumika katika kubadilsiha umeme usio mkondo mnyoofu kwenda katika umeme mkondo mnyoofu.

Inveta ni kifaa kitumikacho kubadilisha umeme mkondo mnyoofu kwenda katika umeme usio mkondo mnyoofu. Hii inafanyika ili kuweza kutumia umeme kirahisi katika vifaa vya umeme ambavyo vingi vinatumia umeme usio mkondo mnyoofu, yaani a.c. Baada ya umeme kubadilishwa basi unaweza kupoozwa ama kupaishwa kirahisi kwa kutumia transfoma , hili haliwezi kufanyika katika umeme mkondo mnyoofu. Ni muhimu kutambua kwamba katika ubadilishaji kiasi cha nusu ya umeme kinapotea na kwa kuwa inveta haina ufanisi wa asilimia mia moja.

Voltimita ni kifaa kinachotumika kupima volti katika sakiti ya umeme. Ili kupima volti, voltimita huwekwa sambamba na sehemu ama chombo kinachoitajika kupimwa volti zake. Volti zinaweza kuweka katika moja ya elfu moja, yaani mV, moja mara, yaani 1×V, 10×V n.k. Lakini katika siku za usoni voltimita zinashindwa umaarufu na maltimita na zinaanza kupotea ama kupatikana kwa shida. Hii ni kwa sababu maltimita inafanya kazi nyingi zaidi, kwa mfano kupima kiasi cha mkondo wa umeme, kapasitensi na volti.

Kinuupepo ni mashine ya kufua umeme kwa kutumia msukumo wa upepo. Hapo zamani, vinuupepo vya kwanza vilikuwa vikitumika katika usagaji wa nafaka na pia kuendesha pampu za kufyonza maji na kukausha maeneo yasiyo makavu. Katika siku za usoni vinuupepo vimekuwa maarufu sana kutokana na kuzalisha nishati hai ya umeme. Hii inasaidi kupunguza alama ya hewa ya ukaa. Kinuupepo cha kufua umeme kinajumuisha mapanga yanayozungushwa na upepo ambayo huzungusha kwanza giaboksi kasha giaboksi huzungusha jenereta. Mzunguko huu huzalisha mkondo wa umeme. Umaarufu mkubwa wa vinuupepo umekuja kutokana na msukumo kuelekea nishati hai.

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.