Mpunga ni aina ya nafaka ambayo baada ya kukobolewa hutoa mchele. Mchele ni chakula maarufu sana hasa katika bara la Asia.
Matumizi[edit | edit source]
Matumizi makubwa ya mpunga ni pamoja na chakula yaani, mchele, malisho ya wanyama, kutoa nishati joto, mboji toka katika mabaki n.k kutegemeana na eneo husika.
Viinilishe[edit | edit source]
Mpunga/mchele huna viinilishe vya wanga kwa kiasi kikubwa na protini kidogo na mafuta katika kiwango kidogo sana.
Kilimo cha mpunga[edit | edit source]
Mpunga hustawi katika maeneo ya mabondeni kwenye udongo hunaotuamisha maji na joto kali (uthibitisho unahitajika). Hivyo mpunga hulimwa zaidi katika maeneo yenye hali ya kitropiki.