Page data
Authors Christopher Sam
Published 2011
License CC-BY-SA-4.0
Impact Number of views to this page. Views by admins and bots are not counted. Multiple views during the same session are counted as one. 150

Maana[edit | edit source]

Mkaa ni aina mojawapo ya fueli inayotokana na kuunguzwa kwa baiomasi bila ya kuwapo kwa oksijeni. Kwa kawaida mkaa una rangi nyeusi. Mkaa ndio chanzo kikuu cha nishati inayotumika majumbani kwa ajili ya kupikia katika miji mingi mikubwa ya nchi zinazoendelea.

Matumizi[edit | edit source]

Mkaa hutumika sana katika kupikia na kwa kiwango kidogo katika kupiga nguo pasi. Pia kuna wakati mkaa unatumika kutoa nishati ya joto hasa maeneo yenye baridi.

Ufanisi wa nishati katika mkaa[edit | edit source]

Ukilinganisha na kuni, mkaa una ufanisi wa juu kidogo. Hii ndio sababu kuu ya wakazi wengi wa mijini kupendelea mkaa zaidi ya kuni. Pia mkaa hutoa kiwango kidogo cha hewa ukaa na masizi ukilinganisha na kuni. Lakini, kutokana na ubunifu na maboresho mbalimbali ya miaka ya karibuni, matumizi ya kuni yanaonekana kufaa zaidi ya mkaa. Hii ni kwa kuwa katika kuipeleka kuni kuwa mkaa, nishati kubwa hupotea katika joto na mwanga. Pia kuna sehemu ya baiomasi huungua kabisa na kuwa majivu. Pia nguvu na muda hutumika katika kutafuta, kukusanya, kukatakata, na kufukia kuni kwa ajili ya kupata mkaa.

Majiko sahihi[edit | edit source]

Katika miaka ya karibuni kumeundwa majiko sahihi ya aina nyingi yanayotumia kuni katika ufanisi mkubwa. Majiko haya hutoa moshi kwa kiwango kidogo sana, yanatoa joto kali na ni rahisi kutengenezwa. Mengi ya majiko haya yanatumia vipisi vidogovidogo vya kuni ama mabaki mengine ya mimea.

Ukurasa huu ni kipisi tafadhali saidia kuendeleza!