Maana[edit | edit source]

Mabadiliko ya tabianchi ni mabadiliko yanayotokea katika maumbo na mifumo ya hali ya hewa. Mabadiliko haya yanaweza kusababishwa na shughuli za binadamu ama njia za asili. Pia mabadiliko haya yanaweza kuwa ya muda mfupi ama mrefu.

Sababu[edit | edit source]

Ukiachana na njia za asili, shughuli za binadamu zinazopelekea hewa mkaa na gesi taka toka viwandani na usafirashaji. Gesi hizi huitwa gesijoto na ndio chanzo kikubwa cha ongezeko la joto duniani.

Viashiria[edit | edit source]

Viashiria vya mabadiliko ya tabianchi ni pamoja na ongezeko la joto duniani, kubadilika kwa ikologia, kuyeyuka kwa barafu katika vilele vya milima, ukame na mafuriko.


Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi katika Kilimo[edit | edit source]

Ili kuongeza mavuno na tija katika sekta ya Kilimo ni vyema kulima mazao na kuendesha kilimo kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi. Hili linaweza kufanyika kwa;

    1. Kulima mazao yanayostahimili ukame
    2. Kupanda mazao ya muda mfupi/mazao yanayokomaa mapema.
    3. Kinga na tahadhari dhidi ya magonjwa na wadudu waharibifu.
    4. Kuzingatia kanuni za kilimo endelevu.
    5. Pia ni vyema kupanda miti kwa wingi ili kupungaza hewa ukaa


Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.