Page data
Authors Christopher Sam
Published 2011
License CC-BY-SA-4.0
Impact Number of views to this page. Views by admins and bots are not counted. Multiple views during the same session are counted as one. 291

Kilimo cha mjini ni aina ya kilimo kinachofanyika mijini na kinaweza kujumuisha ufugaji au ulimaji wa mbogamboga, matunda na mazao ya chakula na pia mazao ya biashara.

Kilimo cha mjini kinaweza kuwa na tija kubwa kwani mbali na kutoa mazao wahusika wanaweza kuongeza kipato kwa kuuza ziada. Mbali na haya kilimo cha mjini ni njia nzuri ya kuboresha afya, yaani mazoezi na mlo kamili.

Katika miji mingi ya Afrika, majiji pia wakazi wengi wanaonekana kujihusisha na kilimo cha mjini, aidha pembezoni ama kwenye vitovu vya miji hiyo.

Pia ni vizuri kufahamu kuwa kama kilimo cha mjini kitafanyika kwa ufanisi na mipango sahihi kinaweza kuwa njia mbadala ya kuleta mandhari nzuri, hewa safi na njia sahihi ya uzungushaji taka.

Ukurasa huu ni kipisi tafadhali saidia kuendeleza!