Inveta ni kifaa kitumikacho kubadilisha umeme mkondo mnyoofu kwenda katika umeme usio mkondo mnyoofu. Hii inafanyika ili kuweza kutumia umeme kirahisi katika vifaa vya umeme ambavyo vingi vinatumia umeme usio mkondo mnyoofu, yaani a.c. Baada ya umeme kubadilishwa basi unaweza kupoozwa ama kupaishwa kirahisi kwa kutumia transfoma, hili haliwezi kufanyika katika umeme mkondo mnyoofu. Ni muhimu kutambua kwamba katika ubadilishaji kiasi cha nusu ya umeme kinapotea kuwa inveta haina ufanisi wa asilimia mia moja.

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.