Hewa safi ni hewa isiyo na vidudu vibaya (germs), isiyokuwa imetumika sana na watu ama wanyama wengine, pia ni hewa isiyo na hewa za sumu.

Tupateje hewa safi?[edit | edit source]

Hewa safi inaweza kupatikana kwa urahisi mbali na miji kama vile shambani, pwani na milimani. Unaweza kwenda kupunga hewa safi katika maeneo haya kama utaamua. Mara nyingi mjini kuna msongamano mkubwa wa watu, wanyama na mashine zitumiazo fueli. Watu na wanyama wote wanahitaji na wanavuta pumzi na mashine zitumiazo fueli, hapa kama vile magari, jenereta n.k, zinatoa hewa za sumu.

Namna ya kupata hewa safi mijini[edit | edit source]

Nyumba zenye madirisha makubwa na yenye kuachwa wazi usiku na mchana ni chanzo kizuri cha hewa safi. Nyumba inapokuwa na madirisha makubwa itaruhusu hewa safi na mwanga wa jua kupita kwa urahisi. Vidudu vingi haviwezi kuishi katika hewa safi na huchukia mwanga wa jua.

Faharasa[edit | edit source]

Rivers-Smith, S. Afya, Macmillan and Co.,Ltd. London, 1966

FA info icon.svg Angle down icon.svg Page data
Authors Christopher Sam
License CC-BY-SA-3.0
Language Kiswahili (sw)
Related 0 subpages, 2 pages link here
Impact 473 page views
Created Mei 20, 2011 by Christopher Sam
Modified Novemba 15, 2022 by Felipe Schenone
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.