Page data
Authors Christopher Sam
Published 2011
License CC BY-SA 4.0
Derivative of Help:Editing
Other derivatives Conceptos básicos
Guia de edição
Inhalt
Language Kiswahili (sw)
Page views 1,717

Angalia Appropedia help kwa ajili ya orodha yenye Makala za msaada.

Kuhariri wiki ni rahisi! Chapa tu ndani kama barua pepe. Kama unahitaji kufanya zaidi, basi soma kurasa ifuatayo chini kwa maelezo juu ya kuumba muonekano. Na unauwezo wa drop us a line na jamii itakusaidia kuunda muonekano kwa ajili yako.

Kuunda kurasa[edit | edit source]

Njia ya haraka zaidi ni kufanya utafutaji kwa kutumia jina jipya kwa kitufe cha Go. Utafutaji usipopata kitu, bofya kwenye kipelekezi chekundu "create this page".

Upaji majina[edit | edit source]

Jina lina hisia za herufi kubwa ama ndogo, isipokuwa kwa herufi ya kwanza, ambayo inatengenezwa yenyewe kuwa herufi kubwa. Usitumie herufi kubwa katika maneno yote, isipokuwa kwa majina maalumu, kwa mfano tunatumia Pampu ya kamba, na sio Pampu Ya Kamba.

Kumbuka kuupa ukurasa wako jina ambalo linaeleza kirahisi makala inahusu nini. Kwa mfanoe "Smithville Local Exchange Trading System" au "SLETS (Smithville Local Exchange Trading System)" au "Smithville local currency scheme" – lolote kati ya haya ni bora zaidi ya "SLETS" tu.

Kwa kanuni juu ya jinsi ya kutoa majina na kurasa za miradi ya aina nyingine, angalia Help:Page naming.

Uundaji muonekano[edit | edit source]

Unaweza kuunda muonekano wa maandishi yako kwa kutumia wiki markup. Njia rahisi ya kufanya hili ni kuchagua maandishi, halafu tumia ufito wa miundo juu ya boksi la kuharir - bofya B kukoleza, kwa mfano. Kuona kitufe kinafanya kazi gani, ning’iniza kipanya juu yake na maandishi yanayoning’inia yatatokea, yanayoelezea kitufe hicho. Lakini unaweza kuunda muonekano mwenyewe, kama utahitaji.

Wiki markup ina herufi za kawaida kama nyota, alama moja za nukuu au alama zenye kazi maalumu ndani ya wiki, mara nyingine kutegemeana na maeneo zilipo. Kwa mfano kuunda muonekano katika italiki, unalijumuisha neno lako ndani ya alama mbili za kunukuu kama ''this''

Aya[edit | edit source]

Appropedia haitambui nafasi za kawaida baina ya mistari. Kuanzisha aya mpya, acha mstari tupu. Unaweza kuanzisha mstari mpya pia kwa alama ya HTML <br>.

Alama za kuunda muonekano[edit | edit source]

Maelezo Unachapa Unapata
inatumika popote
Weka maandishi katika italiki ''italiki'' italiki
Maandishi yaliyokolezwa '''koleza''' koleza
Koleza na weka katika italiki '''''koleza & italiki''''' koleza & italiki
Kubwa <big>KUBWA</big> KUBWA
Ndogo <small>ndogo</small> ndogo
Maandishi ya rangi (choose a color.) <font color="lime">maandishi ya rangi</font> maandishi ya rangi
Ondoka kwenye wiki markup <nowiki>no ''markup''</nowiki> no ''markup''
Signature (tumia hii saini maoni) ~~~~ Username Muda, Tarehe (Eneo)
mwanzoni mwa mstari tu
Vichwa

vya ukubwa tofauti

==ukubwa 1==
===ukubwa 2===
====ukubwa 3====
=====ukubwa 4=====

<!—Yafuatayo chini ni mifano ya sampuli za vichwa zilizoundwa kawaida, kukwepa vipelekezi vya kuhariri.-->

Ukubwa 1


Ukubwa 2

Ukubwa 3

Ukubwa 4

Rula mlalo (tumia kidogo)

----


Orodha nukta


* moja
* mbili
* tatu

 • moja
 • mbili
 • tatu
Orodha ya namba


# moja
# mbili
# tatu

 1. moja
 2. mbili
 3. tatu
Orodha ya maana


;Maana
:kipande 1
:kipande 2

Maana
kipande 1
kipande 2
Maandishi yaliyokwishaundwa

  uwazi kwenye
  mwanzo wa mstari
  unatengeneza
  maandishi yaliyokwishaundwa

uwazi kwenye 
mwanzo wa mstari 
unatengeneza 
maandishi yaliyokwishaundwa
Majedwali

Makala kuu: Help:Tables

{|border="1"
| 1 || 2
|-
| 3 || 4
|}
1 2
3 4

Vipelekezi vya nje[edit | edit source]

Maelezo Unachapa Unapata
Vipelekezi vya ndani [[Kurasa]] Unapata
Piped link [[Kurasa|maandishi mengine]] maandishi mengine
Kipelekezi cha nje http://mediawiki.org http://mediawiki.org
Kipelekezi cha nje,

kichwa tofauti

[http://mediawiki.org MediaWiki] MediaWiki
Kipelekezi cha nje,

hakina jina

[http://mediawiki.org] [1]
Wikipedia

superscript
link

Smithville{{w|Smithville, Northern Elbonia}} SmithvilleW

Hizi ni aina tofauti muhimu mbili za aina ya vipelekezi ndani ya Appropedia: vipelekezi vya ndani kuelekea kurasa nyingine ndani ya wiki - vikujumuisha files (kama picha) na vipelekezi vya nje kuelekea tovuti nyingine.

Kuongeza kipelekezi cha ndani, lifunge jina la kurasa unalotaka kulipelekea ndani ya alama mbili za mabano yenye pembe. Ukihifadhi ukurasa, utaona kipelekezi kipya kinachopelekea kwenye ukurasa wako. Kama ukurasa upo tayari, utaonekana katika maandishi ya bluu, kurasa tupu zinaoneshwa kwa rangi nyekundu.

Herufi ya kwanza ya kurasa inawekwa katika herufi kubwa yenyewe na sehemu wazi zinawakilishwa kwa alama za deshi za chini (kuchapa alama ya deshi ya chini kwenye kipelekezi kunafanya kazi sawa na nafasi wazi, lakini hii haishauriwi).

Vipelekezi vya nje viko katika muonekano wa [http://www.example.org jina la kipelekezi] (ikitoa jina la kipelekezi), ambapo jina la kipelekezi linatofautishwa na na URL kwa nafasi wazi. Vipelekezi bila majina ya vipelekezi vitwekewa namba: [http://www.example.org] inakuwa [1]. Vipelekezi bila ya alama za mabano ya pembe zitaoneshwa kama zilivyo: http://www.example.org .

HTML[edit | edit source]

Baadhi ya alama za HTML zinakubalika kwenye Appropedia, kwa mfano <code>, <div>, <span> and <font>.

Majarada[edit | edit source]

Appropedia inatilia mkazo sana matumizi ya vitu vinavyotia nguvu makala na kuzifanya ziwe na maelekezo zaidi. Vitu vinavyotia nguvu kujifunza katika lugha nyingi vinawekewa mkazo pia. Yaffuatayo ni maelekezo ya namna na jinsi ya kuweka vitu vithibitishi katika kurasa yako.

Upakiaji[edit | edit source]

Kabla ya kupakia, tafadhali hakikisha unayo rights ili kupakia na kusambaza majarada husika na unatoa haki hiyo kwa watu wengine.

 1. Hifadhi jarada kwenye kompyuta yako na kumbuka wapi, yaani folda gani.
 2. Kwenye Appropedia, bofya kipelekezi cha "Upload a file" kilichoko kwenye menyu ya "toolbox" upande wa kushoto
 3. Bofya kitufe cha "Browse..." kwenye ukurasa wa "Upload file" , na peruzi kwenye jarada ulilohifadhi
 4. Lichague jarada hilo
  • Hii itajaza chanzo na jina la mahali kuhusu jarada kwenye sehemu za maandishi zinazotatikana.
 5. Weka maelezo mafupi. (hatua hii sio ya lazima lakini inahusika)
  • Sehemu hii ya maelezo mafupi ni sehemu nzuri ya kueleza kwanini unazo haki za kutuma jarada
 6. Kisha bofya kitufe cha "Upload file" kumalizia upakiaji. Hii itachukua muda kama mtandao wako ni taratibu.

Mionekano inayopendelewa ni JPEG kwa picha za taswira, PNG kwa michoro na taswira zingine, na OGG kwa sauti. Tafadhali yape majina majarada yako kimaelezo kuepuka kuchanganyikiwa.

Tafadhali tambua kuwa kuhusu kurasa za wiki, wengine wanauwezo wa kuhariri uliyopakia (na watawala wanweza kuyafuta) kama watadhani yanasaidia mradi, na unaweza kufungiwa kupakia kama utadhuru mfumo.

Baada ya jarada lako kupakiwa unaweza ukataka kuweka kwenye kurasa yako put it in your page.

Epuka majarada makubwa ya picha[edit | edit source]

Majarada makubwa ya picha lazima yaepukwe – yaweka mzigo kwenye seva na yanasababisha kurasa zipakuliwe taratibu (na hasa kwenye maeneo ya mbali na yasiyo na maendeleo). Kwa kawaida majarada yanabidi yaminywe kubaki na 200 kB au pungufu (1 MB au pungufu ni picha kubwa na yenye vitu vingi). Picha ghafi toka kamera za digitali zinaweza kuwa na zaidi ya 5 MB, ambayo ni kubwa sana.

Kifaa cha kuhariri picha kinaweza kuifanya iwe ndogo. Programu nzuri sana ya bure kwa watumiaji wa Windows ni Faststone.Hapa ni some instructions for the mac, majarada haya yanasemekana ni makubwa kidogo, lakini yatafaa..

Kuweka picha[edit | edit source]

Kuweka picha yako (jarada) kwenye kurasa yako, unaipelekea kwake kwa kuweka alama mbili za mabano kuzunguka jina la ukurasa wa jarada (kama vile ni kurasa nyingine ya Appropedia ). Kwa mfano kama umepakia jarada lenye jina AEFprevfilt2.jpg, utaweka alama mbili za mabao kuzunguka image:AEFprevfilt2.jpg.

Maelezo Unachapa Unapata
Picha tuu [[Image:AEFprevfilt2.jpg]] AEFprevfilt2.jpg
Vibandiko [[Image:AEFprevfilt2.jpg|thumb]]
AEFprevfilt2.jpg
Vibandiko na kichwa [[Image:AEFprevfilt2.jpg|thumb|Fig 1: Kusafisha chujio lililozeeka]]
Fig 1: Kusafisha chujio lililozeeka
Vibandiko na
kichwa na mahali
[[Image:AEFprevfilt2.jpg|thumb|left|Fig 1: Kusafisha chujio lililozeeka]]
Fig 1: Kusafisha chujio lililozeeka
Gallery <gallery>
Image:AEFprevfilt2.jpg|Fig 1: Kusafisha chujio lililozeeka
Image:AEFprevfilt2.jpg|Fig 1a: Itakuwa ni nzuri kama ni picha ya tofauti
Image:AEFprevfilt2.jpg|Fig 1b: Itakuwa ni nzuri kama ni picha ya tofauti
</gallery>

Angalia wikipedia:Wikipedia:Picture tutorial kwa ajili ya chaguzi zaidi.

Kuweka video[edit | edit source]

Vipengele[edit | edit source]

Kuongeza ukurasa katika kipengele, chapa [[Category:Jina la kipengele]] chini ya kurasa.

Vipengele kwenye Appropedia vinatumika kupangilia maudhui. Kwa mfano kama kuna makala nyingi juu ya mada maji, basi inaleta maana kutengeneza kipengele kuhusu maji.

Kutengeneza kipengele kiitwacho Maji chapa https://www.appropedia.org/Category:Maji kwenye ufito wa anuani

Kuweka kipelekezi kwenye Kipengele cha maji (kipelekezi kionekanacho, na sio kuongeza ukurasa katika kipengele hicho) chapa [[:Kipengele:Maji]] . Kama utahitaji kipelekezi kionekane kwa maandishi tofauti, chapa [[:Kipengele:Maji | LINKTEXT]] ambapo LINKTEXT ni maandishi yatakayoonekana kwenye kipelekezi.

Kuangalia mti wa vipengele angalia Appropedia:Mti wa Vipengele. Inasaidia kuwa na mti wa vipengele umefunguliwa kwenye kitufe kingine wakati ukihariri kurasa na kuamua vipengele sahihi zaidi.

Hatua iliyofikiwa[edit | edit source]

Kwenye kurasa za miradi ni vizuri kueleza hatua iliyofikiwa. Mara nyingi gharama za kutengeneza upya au kujenga teknolojia sahihi ni kubwa. Kumudu gharama hii, kwanza, lazima kuwe na maelezo ya kutosha na michoro ili watumiaji waamini kwamba kuna umakini wa kutosha kwenye ubunifu bidhaa na kwamba kifaa kilichobuniwa kitafanya kazi kama kilivyoelezewa. Pili, lazima kuwe na historia ya mafanikio katika utumiaji wa bidhaa kabla ya uwekezaji wa muda na malighafi katika ugunduzi. Kwa kufata maelekezo kwenye ukurasa wa Status, hatua ya teknolojia sahii Fulani inaweza kuoneshwa kirahisi kusaidia watumiaji jinsi ya kutumia teknolojia hiyo.

Maelezo zaidi[edit | edit source]

Angalia Category:Appropedia help for other specific help topics. Angalia pia Wikipedia:How to edit a page na Wikipedia:Help:Contents/Editing Wikipedia.

Kama una swali la kiufundi ambalo alijajibiwa hapa, unaweza kuhitaji kuangalia help pages on Wikipedia (kwa kuwa Appropedia na Wikipedia zinatumia mfumo laini mmoja); au tafadhali uliza kwenye ukurasa wa Technical questions au kwenye Village pump – tutakuwa na furaha kusaidia!

Vipelekezi vya nje[edit | edit source]

Viongazaji[edit | edit source]


Tutorials[edit | edit source]