Baiogesi ni gesi inayozalishwa kutokana na mvunjiko wa kibaiolojia wa vitu vya kioganiki bila kuwako na oksijeni. Baiogesi ni fueli. Baiogesi inaundwa na gesi kuu mbili, ambazo ni methane na hewa ukaa. Gesi nyingine ni kama vile haidrojeni, nitrojeni na nyingine katika kiwango kidogo sana. Uzalishwaji wa baiogesi ni mchakato wa kibaiolojia kwani unawezeshwa na viumbe hai vidogo bila kuwapo na oksijeni. Mchakato huu unafahamika kama mmeng'enyo wa kianaerobiki wa vitu kama baiomasi, mbolea, taka, maji kijani na vitu vya mimea. Baiogesi inazalishwa kutokana na vitu vya kioganiki, yaani mimea na wanyama.

Uzalishaji wa baiogesi[edit | edit source]

Uzalishaji wa baiogesi unafanyika katika njia kuu mbili zifuatazo. i) Uchimbaji wa gesi asilia ardhini na ii) kuandaa na kufyonza baiogesi.

Uchimbaji wa gesi asilia toka ardhini[edit | edit source]

Baadhi ya sehemu za dunia zimekusanya mabaki ya kioganiki. Bahari zimekusanya mabeki mengi ya kioganiki toka katika ardhi. Hii ndiyo sababu kiwango kikubwa cha gesi asilia kuchimbwa chini ya bahari au karibu na pwani. Pia kiasi kikubwa cha mabaki ya kioganiki yapo ardhini. Gesi asilia inapatikana chini ya miamba isiyopitisha maji. Ufyonzaji wa gesi asilia toka ardhini unahusisha kutoboa miamba na kuweka mabomba pale gesi asalia inapofikiwa. Baada ya kufyonzwa gesi asilia uhifadhiwa katika makaro makubwa. Kisha uchakachuliwa na kusambazwa kwa watumiaji. Gesi asilia ina asalimia 80 methane na asilimia 15-20 za hewa ukaa. Wingi huu wa methane unaifanya gesi asilia kuwa bora zaidi ya baiogesi inayotokana na taka za wanyama/mbolea.

Uandaaji na uzalishaji wa baiogesi[edit | edit source]

Baiogesi inaweza kuandaliwa na kuzalishwa nyumbani kwa kutumia kinyesi cha ng'ombe. Baiogesi hapa inazalishwa kwa tanki la baiogesi

Uzalishaji wa baiogesi nyumbani[edit | edit source]

Mchanganyiko wa mbolea ya ng'ombe, mboga za majani, na mabaki mengine ya kioganiki yanawekwa katika tanki la baiogesi na kuachwa kwa muda ili kuchachuka. Matanki haya yanafungwa kwa umahiri kuzuia hewa kuingia ndani ya tanki la baiogesi...

Hewa ukaa inaondolewa kwa kuipitisha katika maji ya chokaa/lime water. Haidrojeni salfaidi inaondolewa kwa kupitishwa katika chembechembe za chuma/iron fillings. Na mwishowe baiogesi inapitishwa katika kalsiamu kloraidi kufyonza mvuke. Hii ifanyike baada ya hatua mbili hapo juu. Baiogesi hupungua kulingana na matumizi hivyo ni lazima mbolea ibadilishwe na mpya.

Muhimu[edit | edit source]

Kumbuka kuwa nusu kilo ya mbolea ya ng'ombe inaweza kuzalisha lita 25 za baiogesi ambazo zinaweza kutumika kupikia milo 3 kwa watu 4 mpaka 6 wa familia. Na lita 1,700 za baiogesi zina nishati sawa na lita 1 ya mafuta ya petroli.

Matumizi[edit | edit source]

Kupasha joto kwa ajili ya mapishi, kukausha, joto n.k. Kuzalisha umeme kupitia jenereta. Fueli katika injini. Malighafi katika uzalishaji wa kemikali, plastiki, rangi, mbolea, madawa na milipuko.

Madhara[edit | edit source]

Uchafuzi wa hewa, kuongezeka kwa joto duniani na kutoboka kwa ozoni (uthibitisho unahitajika).

Discussion[View | Edit]

Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.