Page data
Published 2011
License CC-BY-SA-4.0
Impact Number of views to this page. Views by admins and bots are not counted. Multiple views during the same session are counted as one. 126

Biofueli ni fueli inayopatikana kutokana na masi ya mimea au viumbehai vingine. Tofauti na fueli kisukuku ambayo ni mabaki ya viumbehai ya miaka mingi iliyopita biofueli hutokana na masi iliyopatikana hai au iliyokaa muda kidogo tu. Biofueli hupatikana kama dutu mango, kiowevu au gesi.

Matumizi ya biofueli ni kama nishati ya kuendesha injini za magari, kuwasha moto nyumbani au upishi. Hutumiwa pia kwa utengenezaji wa umeme.

Kuna mbinu mbili hasa kutengeneza biofueli.

  • kulima mimea yenye kiwango kikubw cha sukari au wanga kama muwa. Kwa msaada wa bakteria wanga au sukari hubadilishwa kuwa alikoholi (ethanoli).
  • kulima mimea yenye kiwango kikubwa cha mafuta katika mbegu au miili yao kama algae, michikichi (mawese) au soya.

Ethanoli hizi hutumiwa badala ya petroli na mafuta badala ya diseli katika injini ya mwako.

Njia nyingine ni kutumia ubao au manyasi mbalimbali zinazokaushwa, mara nyingi kukatwa na kupewa umbo la donge halafu kuchomwa kwa kutengeneza umeme.

Mifano[edit | edit source]

Jatropha

Mabaki ya mafuta ya kula

Usomaji zaidi[edit | edit source]

Nishati hai

Baiogesi

Ukurasa huu ni kipisi tafadhali saidia kuendeleza!