Nchi zinazoendelea ni nchi zilizo na uchumi duni, kipato duni, miundombinu duni na huduma za jamii duni. Nchi zinazoendelea pia zinajulikana kama nchi za dunia ya tatu. Lakini kwa kuwa nchi zinazoendelea ziko nyingi kuliko nchi zilizoendelea kumekuwa na msukumo wa kutaja nchi zinazoendelea kama nchi nyingi duniani. Yaani wengi wanadhani ni vizuri
kuzitaja nchi hizi kwa uhalisia na sio kwa kile kinachokosekana. Pia sio sahihi sana kutaja nchi zinazoendelea kama nchi za kusini kwani kuna baadhi ya nchi ziko kusini mwa dunia na zina maendeleo halikadhalika ziko nchi kaskani mwa dunia na zina maendeleo duni.