Kinuupepo ni mashine ya kufua umeme kwa kutumia msukumo wa upepo. Hapo zamani, vinuupepo vya kwanza vilikuwa vikitumika katika usagaji wa nafaka na pia kuendesha pampu za kufyonza maji na kukausha maeneo yasiyo makavu. Katika siku za usoni vinuupepo vimekuwa maarufu sana kutokana na kuzalisha nishati hai ya umeme. Hii inasaidi kupunguza alama ya hewa ukaa. Kinuupepo cha kufua umeme kinajumuisha mapanga yanayozungushwa na upepo ambayo huzungusha kwanza giaboksi kasha giaboksi huzungusha jenereta. Mzunguko huu huzalisha mkondo wa umeme. Umaarufu mkubwa wa vinuupepo umekuja kutokana na msukumo kuelekea nishati hai.

FA info icon.svg Angle down icon.svg Page data
License CC-BY-SA-3.0
Language Kiswahili (sw)
Related 0 subpages, 0 pages link here
Impact 370 page views
Created Mei 22, 2011 by Christopher Sam
Modified Novemba 15, 2022 by Felipe Schenone
Cookies help us deliver our services. By using our services, you agree to our use of cookies.